Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA78

MKUTANO WA 78 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA78

Jukwaa  limeandaliwa kwa ajili ya mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati ulimwengu ukiendelea kukabiliwa na mdororo wa kijamii na kiuchumi kutokana na Covid 19 na athari zinazoendelea za vita nchini Ukraine, mjadala utafanyika kikamlifu ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019, na viongozi wa ulimwengu wakielekea NY kuwasilisha kauli zao katika Ukumbi mashuhuri. 

Hapa, Habari za UN inakupa kiti cha mstari wa mbele katika shughuli zote. Katika simu yako ya mkononi au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapofafanua hatua dhidi ya changamoto kubwa zaidi duniani na kushiriki katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hatua kabambe ya kumaliza janga la tabianchi, na vikao vitatu vya ngazi ya juu visivyo na kifani kuhusu afya: maandalizi dhidi ya majangahuduma ya afya kwa wote; na mapambano ya kimataifa dhidi ya kifua kikuu

Tutembelee kwenye majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

Twitter: twitter.com/HabarizaUN

Youtube: https://www.youtube.com/@UNNewsKiswahili 

Phiona anafanya kazi katika kituo cha afya nchini Uganda kama mwanaharaki wa rika ya akina mama, anasaidia kutoa mafunzo na kusaidia akina mama kujifungua watoto wasio na VVU.
© UNICEF/Karin Schermbrucker

Viongozi wa dunia na wadau washikamana kutaka fursa sawa ya huduma za afya kwa wote: UNITAID

Wakati wa mkutano mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wa mwaka huu, viongozi wa dunia, wadau wa afya na wawakilishi wa jamii wanaungana na shirika la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu UNITAID, kutoa wito wa upatikanaji wa haraka na usawa zaidi wa bidhaa za afya zinazookoa maisha ili kuendeleza mchakato wa kupambana na changamoto kubwa zaidi za leo za afya, ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi ya mama na mtoto, kuzuia majanga, kujiandaa na hatyua za kukabiliana na majanga, na virusi vya ukimwi VVU, kifua kikuu na malaria.

19 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Leo ni siku ya pili na ya mwisho wa mkutano kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs lakini leo pia ndio pazia la mjadala Mkuu wa 78, UNGA78 limefunguliwa na pamoja na na hotuba za viongozi pia kutakuwa na mikutano itakayo jadili hali za ulinzi na usalama katika mataifa mbalimbali na hapo kesho kutakuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Sudan. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na nashinani ikimulika hotuba za viongozi katika Baraza Kuu na kazi za vijana katika utekelezaji wa DGs.  

Sauti
11'34"
© FAO/Jeanette Van Acker

Mazao ya asili yaliyo puuzwa yatasaidia kutokomeza njaa

Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030

Wadau wa Maendeleo wamejaa hapa katika makao Makuu hakika na rangi za malengo 17 zikiwa zimetaradadi kila kona kuanzia nje mpaka ndani ya Baraza Kuu, mwaka huu wakija na maudhui yasemayo, Kujenga upya kuaminiana na kuchochea mshikamano wa dunia.

Sauti
2'17"
Mkutano wa SDG unaendelea katika ukumbi wa Baraza Kuu kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
UN Photo/Cia Pak

Badala ya kutomwacha yeyote nyuma tunahatarisha kuyaacha malengo ya SDGs nyuma: Guterres

Muda wa kuchukua hatua ni sasa kuhakikisha tunayaokoa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanasuasua na kuwa kwenye hatari kubwa ya kutotimizwa amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika ufunguzi wa jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDG linaofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa  jijini New York Marekani chini ya mwamvuli wa Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78.