Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA78

MKUTANO WA 78 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA78

Jukwaa  limeandaliwa kwa ajili ya mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati ulimwengu ukiendelea kukabiliwa na mdororo wa kijamii na kiuchumi kutokana na Covid 19 na athari zinazoendelea za vita nchini Ukraine, mjadala utafanyika kikamlifu ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019, na viongozi wa ulimwengu wakielekea NY kuwasilisha kauli zao katika Ukumbi mashuhuri. 

Hapa, Habari za UN inakupa kiti cha mstari wa mbele katika shughuli zote. Katika simu yako ya mkononi au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapofafanua hatua dhidi ya changamoto kubwa zaidi duniani na kushiriki katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hatua kabambe ya kumaliza janga la tabianchi, na vikao vitatu vya ngazi ya juu visivyo na kifani kuhusu afya: maandalizi dhidi ya majangahuduma ya afya kwa wote; na mapambano ya kimataifa dhidi ya kifua kikuu

Tutembelee kwenye majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

Twitter: twitter.com/HabarizaUN

Youtube: https://www.youtube.com/@UNNewsKiswahili 

UN News

Tuna imani Tanzania tutafikia lengo la huduma za afya kwa wote 2030: Waziri Ummy

Tanzania taifa lililo Afrika Mashariki limesema limejipanga vyema katika kutekeleza azimio la kuchukua hatua kuhusu huduma za afya kwa wote lililoidhinishwa kwa kauli moja mwishoni mwa juma na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alikuwa miongoni mwa waliohudhuria na ameketi chini na Flora Nducha wa Idhaa hii na kumfafanulia mikakati yao ya kutekeleza azimio hilo.

Sauti
5'52"