Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Wanawake

Mjasiriamali Mwanamke Haika Lawere anayemiliki hoteli ya Mbezi Garden jijini Dar Es Salaam Tanzania.
© World Bank

Bisha hodi Mbezi Garden nchini Tanzania uone manufaa ya mradi wa We-Fi wa Benki ya Dunia na wadau

Mpango wa Ufadhili Wajasiriamali Wanawake, (We-Fi) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na wadu umewezesha biashara kukwamuka nchini Tanzania baada ya janga la COVID-19, hatua ambayo imeinua pia jamii nzima na si wajasiriamali wanawake peke yao. Simulizi hii ya Assumpta Massoi inamulika mjasiriamali mwanamke Haika Lawere anayemiliki hoteli ya Mbezi Garden jijini Dar Es Salaam ambako ni jiji kuu la biashara la taifa hilo la Afrika.

Sauti
2'45"
Mradi wa "Chaguo Langu Haki Yangu" umewawezesha wanawake na wasichana na kuwasaidia kuondokana na mila potofu ya ukeketaji na ndoa za utotoni nchini Tanzania.
© UNFPA

Mnufaika wa mradi unaotekelezwa na UNFPA Tanzania aelezea jinsi ulivyomtoa machozi

Mpango wa “Chaguo Langu, Haki Yangu” nchini Tanzania ni jitihada thabiti zinazolenga kuwawezesha wanawake na wasichana kuishi maisha huru dhidi ya ukatili na vitendo hatarishi. Kwa ufadhili wa Serikali ya Finland, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la IPS, linafanya mabadiliko halisi katika jamii. 

Sauti
2'54"
Mnufaika wa mpango wa UN Women nchini Tanzania anatumia jiko bora lililoboreshwa ambalo limepunguza kwa kiasi kikubwa muda anaotumia kupika chakula.
© UN Women

Kulea ni jukumu la kila mtu na kunabadilisha maisha Afrika Mashariki na Kusini

Kote Afrika Mashariki na Kusini, mamilioni ya wanawake huanza siku zao mapema sana kabla hata ya jua kuchomoza. Huteka maji, huandaa chakula, kuwalea watoto na wazee, kusaidia wanajamii wenye ulemavu na kuhakikisha familia zinaendelea kama kawaida. Kazi hii ya huduma isiyolipwa ndio inayoshikilia uchumi kuendelea kuimarika lakini inakuja na gharama kubwa. Wanawake wanapata upungufu wa muda, mapato kidogo, na afya duni.