Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iwe ni baraka au laana, maendeleo ya AI yanakwenda kwa kasi ya radi, tumakinike: Israel

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihutubia mjadala mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 78 mjini New york.
UN Photo/Cia Pak
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihutubia mjadala mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 78 mjini New york.

Iwe ni baraka au laana, maendeleo ya AI yanakwenda kwa kasi ya radi, tumakinike: Israel

Masuala ya UM

Endapo kutakuwa na ushirikiano wa dhati baina ya mataifa mengine ya nchi za Kiarabu na Israel basi Amani baina ya Israel na Palestina baina ya uzao wa Isac na Ismail itawezekana. Ndivyo alivyoanza hotuba yake waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihutubia mjadala mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii leo mjini New york. 

Amesisitiza kuwa Amani baina ya Israel na Sauri Arabia itakuwa daraja la kujenga Mashariki ya Kati mpya na kubadili eneo zima la Mahsraiki ya Kati na kuvunja ukuta wa chuki uliojenge kwa muda mrefu.

Tweet URL

Amesema na hilo pekee litaweka historia ya kuunganisha Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na Israel. “Amani inaweza kupatikana tu endapo msingi wake ni ukweli, haiwezi kutokana na uongo na haiwezi kutokana na kutowatambua Wayahudi.”

Ametoa wito kwa uongozi wa Palestina kutosambaza chuki dhidi ya Wayahudi na taifa lao.

Na kisha akageukia suala la Iran na nyuklia ambapo ametoa wito wa vikwazi kuongezwa na kulibana taifa hilo ili lisiwe mmiliki wa sialaha za maangamizi za nyukia na kuahidi kwamba wakati wote atakapokuwa waziri mkuu wa Israel  atafanya kila liwezekano kuhakikisha Iran haitomiliki silaha za nyuklia kwani sio tu tishio kwa Israel bali kwa dunia nzima.

Kasi ya maendeleo ya AI ni tishio kwetu sote

Bwana Netanyahu ametumia dakika nyingi za hotuba yake kuelezea madhara yatakayopatikana kwa Dunia endapo maendeleo ya akili mnemba au AI hayatodhibitiwa na kuwa ya faida badala ya hasara kwa Dunia.

Ametoa wito wa mshikamano kwa Dunia nzima na kufanya kazi pamoja kuhakikisha maendeleo ya akili mnemba au AI yanakuwa baraka na sio laana, yanaleta faida na sio hasara kwa dunia na watu wake ameonya kwamba “ Maendeleo ya akili mnemba yanakwenda kwa kasi ya radi, ilichukua karne na karne kukabiliana mapinduzi ya kilimo, ilichukua miongo kukabiliana mapinduzi ya viwanda lakini tunaweza kuwa na miaka michache kukabiliana na mapinduzi ya akili mnemba, changamoto zake ni kubwa na ziko mbele yetu, kudanganywa kwa akili, kupoteza ajira, kuongezeka kwa uhalifu na na kudukua mifumo yote inayowezesha maisha ya sasa. Na kinachosumbua zaidi ni uwezekano wa vita vinavyosukumwa na AI vinavyoweza kufikia kiwango kisichoelezeka.”

Ameendelea kusema na tishio kubwa zaidi uwezekano wa mashine za AI kudhibiti binadamu badaya wanadamu kudhibiti mashine hizo.

Amesema lakini AI ikitumika vyema Dunia inaweza kufika ambako haijawahi kufikiria, mathalani teknolojia hiyo kusaidia kuhudumia wagonjwa, kutatua changamoto zingine za kimataifa na kufanya Maisha kuwa bora zaidi. 

Hivyo ametoa wito kwa viongozi wote wa dunia kushirikiana kuhakikisha kuwa “AI inaleta uhuru zaidi na sio kuupunguza, kuzuia vita badala ya kuvianzisha na kuhakikisha kuwa watu wanaishi Maisha marefu zaidi, wanazalisha zaidi na Maisha ya Amani zaidi kwani inawezekana “

Bofya hapa kutazama hotuba yake.