Masuala ya UM

Ushirika wa Kusini- Kusini ni nini? Na ni kwa nini una umuhimu?

Juma hili katika mji mkuu wa Argentina Buenos Aires, watu zaidi ya 1000 wanakutana ikiwemo wawakilishi wan gaizi ya juu wa serikali na wawakilishi kutoka sekta binafsi na asasi za kiraia kwa ajili ya mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa ambao ni wa ngazi ya juu kuhusu ushirika wa Kuisni-Kusini au BAPA+40

Mamlaka Zanzibar wapongeza programu ya kujitolea ya UN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameipongeza azma ya Umoja wa Mataifa (UN) kupitia programu yake ya kujitolea ya Umoja huo (UNV) kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika shughuli za maendeleo.

WFP na serikali wachunguza madai ya kutiwa sumu katika chakula cha WFP Uganda.

Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP) linashirikiana na serikali ya Uganda kuchunguza kilichosababisha kuugua kwa watu zaidi ya 282 baada ya kupokea msaada wa chakula aina ya nafaka kutoka kwa WFP.

Kuna hatua katika kupambana na unyanyasaji na ukatili wa kingono UN

Umoja wa Mataifa umeorodhesha visa 259 vya madai ya unyanyasaji na ukatili wa kingono (SEA) mwaka 2018 kwa mujibu wa ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres iliyowasilishwa leo kwenye Baraza JKuu la Umoja huo. Ingawa idadi ya visa imeongezeka ikilinganishwa na miaka miwli iliyopita , ripoti inaonyesha ongezeko la uelewa miongoni mwa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wanaohusiana na Umoja wa Mataifa , na kumekuwa na nyenzo zilizoboreshwa za kutoa tarifa katika mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa.

Pamoja na hatua ilizopiga, DRC bado inahitaji kusaidiwa- Leila Zerrougui

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao maalum mjini New York Marekanikujadili hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini DRC ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa  Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO , Leila Zerrougui amewaeleza wajumbe kuhusu hali ya sasa ya DRC.

Guterres aelezea kusikitishwa na vifo kutokana majanga Indonesia huku akitoa mshikamano kwa mamlaka.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kusikitishwa kwake na vifo, uharibifu wa mali na kufurushwa kwa watu kufuatia mafuriko na tetemeko la ardhi huko Sentani, Jayapura na Papua magharibi mwa jimbo la Tenggara nchini Indonesia.

Kukaa gerezani muda mrefu bila kuhukumiwa si haki-UNODC

Maofisa wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambamba na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC wiki hii wanafanya ziara katika Kaunti ya Lamu nchini Kenya kwa lengo la kusaidia kutafuta haki kwa watu waliokaa magerezani kwa muda mrefu zaidi ikilinganishwa na makosa waliyoyatenda au kuchelewa kwa hukumu zao. 

Guterres aelezea kusikitishwa na madhara ya kimbunga Idai, WFP yajizatiti kuwasilisha misaada

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kusikitishwa kwake na vifo, uharibifu wa mali na kufurushwa kwa watu kufuatia mvua kubwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Idai.

Mladenov alaani ukatili unaoelekezwa dhidi ya waandamanaji na vikosi vya Hamas Gaza

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mchakato wa amani huko Mashariki  ya Kati Nickolay Mladenov amelaani vikali kampeni ya kamatakamata na ukatili unaotumiwa na vikosi vya Hamas dhidi ya waandamanaji ikiwemo wanawake na waoto huko Ukanda wa Gaza katika kipindi cha siku tatu zilizopita.

UN yakumbuka wafanyakazi wake waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege Ethiopia

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika tukio maalum la kukumbuka wafanyakazi 21 wa umoja huo waliofariki dunia kwenye ajali  ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia, iliyotokea huko Addis Ababa Ethiopia Jumapili iliyopita.