Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA78

MKUTANO WA 78 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA78

Jukwaa  limeandaliwa kwa ajili ya mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati ulimwengu ukiendelea kukabiliwa na mdororo wa kijamii na kiuchumi kutokana na Covid 19 na athari zinazoendelea za vita nchini Ukraine, mjadala utafanyika kikamlifu ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019, na viongozi wa ulimwengu wakielekea NY kuwasilisha kauli zao katika Ukumbi mashuhuri. 

Hapa, Habari za UN inakupa kiti cha mstari wa mbele katika shughuli zote. Katika simu yako ya mkononi au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapofafanua hatua dhidi ya changamoto kubwa zaidi duniani na kushiriki katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hatua kabambe ya kumaliza janga la tabianchi, na vikao vitatu vya ngazi ya juu visivyo na kifani kuhusu afya: maandalizi dhidi ya majangahuduma ya afya kwa wote; na mapambano ya kimataifa dhidi ya kifua kikuu

Tutembelee kwenye majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

Twitter: twitter.com/HabarizaUN

Youtube: https://www.youtube.com/@UNNewsKiswahili 

Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Isdor Mpango akihutubia katika mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. (21 Sept 2023).
UN Photo/Cia Pak

‘Jicho kwa jicho, huacha kila mtu kipofu’ – Makamu wa Rais wa Tanzania katika UNGA 78

Msemo wa wahenga, “Jicho kwa jicho huacha kila mtu kipofu” umepata nafasi katika ukumbi maarufu wa kihistoria wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa nchini Marekani pale ambapo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango ameutumia msemo huo akisisitiza amani ulimwenguni alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa saa za jioni jijini New York.

Rais William Samoei Ruto wa Jamhuri ya Kenya akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 78 cha Baraza Kuu.
UN Photo/Cia Pak

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lifanyiwe marekebisho - Rais Ruto

Takwa la muda mrefu la viongozi wengi hususani kutoka Barani Afrika la Baraza la Usalama la Umoja wa lililoundwa tarehe 25 Octoba mwaka 1945 kufanyiwa marekebisho makubwa limeendelea kuchukua nafasi katika hotuba za viongozi wa ngazi za juu wanaohutubia katika mkutano wa 78 wa Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo hii leo Rais wa Kenya amesema sababu zote za kulifanyia marekebisho zipo wazi. 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Dambudzo Mnangagwa wakati akihutubia mkutano wa 78 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani
UN Photo/Cia Pak

Acheni kutumia vikwazo vya kimataifa kama silaha - Rais Mnangangwa

“Tunalaani vikwazo vinavyowekwa na nchi tajiri kwa nchi kama zimbabwe na Cuba ambavyo ni haramu na vinatumiwa kama nyenzo ya sera za kigeni ya mataifa tajiri kwani vikwanzo hivyo vinatatiza uaminifu, mshikamano na umoja wa kimataifa.“ Amesema leo Rais wa Zimbabwe Emmerson Dambudzo Mnangagwa wakati akihutubia mkutano wa 78 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakifanya doria ya usiku huko Bentiu, Sudan Kusini.
UNMISS/Gregório Cunha

Habari kwa ufupi na yanayoendelea UNGA78

Leo ni siku ya tatu ya mjadala mkuu wa mabaraza kuu la Umoja wa Mataifa UNGA78 ambapo wakuu wa nchi na serikali wanaeendelea kutoa hotuba zao kutathimini changamoto na hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa ajenda za Umoja wa Mataifa, na miongoni watakaopanda katika mimbari leo kutoka Afrika ni Rais wa Kenya, Burundi, Sudan Kusini, Zimbabwe, Malawi, Sudan na makamu wa Rais wa Uganda na Tanzania.

UN News

Tunaelimisha wanafunzi na vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi - Madina Jubilate Kimaro

Wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Madina Jubilate Kimaro, Balozi wa Mazingira wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Tanzania.

Sauti
6'24"

21 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi.

Sauti
12'28"