Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA78

MKUTANO WA 78 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA78

Jukwaa  limeandaliwa kwa ajili ya mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati ulimwengu ukiendelea kukabiliwa na mdororo wa kijamii na kiuchumi kutokana na Covid 19 na athari zinazoendelea za vita nchini Ukraine, mjadala utafanyika kikamlifu ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019, na viongozi wa ulimwengu wakielekea NY kuwasilisha kauli zao katika Ukumbi mashuhuri. 

Hapa, Habari za UN inakupa kiti cha mstari wa mbele katika shughuli zote. Katika simu yako ya mkononi au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapofafanua hatua dhidi ya changamoto kubwa zaidi duniani na kushiriki katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hatua kabambe ya kumaliza janga la tabianchi, na vikao vitatu vya ngazi ya juu visivyo na kifani kuhusu afya: maandalizi dhidi ya majangahuduma ya afya kwa wote; na mapambano ya kimataifa dhidi ya kifua kikuu

Tutembelee kwenye majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

Twitter: twitter.com/HabarizaUN

Youtube: https://www.youtube.com/@UNNewsKiswahili 

UN News/Assumpta Massoi

Vijana tusiwe watazamaji bali tuchukue hatua kwa kuanza na tulicho nacho- Emmanuel

Vijana wana dhima kubwa katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayofikia ukomo mwaka 2030. Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi hiyo ya vijana wanatumia vijana wenyewe ili wawe mabalozi wa mashirika hayo mashinani ili kupigia chepuo yale yaliyomo kwenye SDGs. Mathalani nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lina mabalozi na miongoni mwao ni Emmanuel Cosmas Msoka yeye akijikita kwenye masuala ya usafi wa maji, usafi wa mazingira (WASH) na ubunifu.

Sauti
3'33"