Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA78

MKUTANO WA 78 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA78

Jukwaa  limeandaliwa kwa ajili ya mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati ulimwengu ukiendelea kukabiliwa na mdororo wa kijamii na kiuchumi kutokana na Covid 19 na athari zinazoendelea za vita nchini Ukraine, mjadala utafanyika kikamlifu ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019, na viongozi wa ulimwengu wakielekea NY kuwasilisha kauli zao katika Ukumbi mashuhuri. 

Hapa, Habari za UN inakupa kiti cha mstari wa mbele katika shughuli zote. Katika simu yako ya mkononi au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapofafanua hatua dhidi ya changamoto kubwa zaidi duniani na kushiriki katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hatua kabambe ya kumaliza janga la tabianchi, na vikao vitatu vya ngazi ya juu visivyo na kifani kuhusu afya: maandalizi dhidi ya majangahuduma ya afya kwa wote; na mapambano ya kimataifa dhidi ya kifua kikuu

Tutembelee kwenye majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

Twitter: twitter.com/HabarizaUN

Youtube: https://www.youtube.com/@UNNewsKiswahili 

Csaba Kőrösi (kushoto) Rais wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la UN akikabishi rungu la kuongoza mkutano kwa Rais wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la UN (UNGA78). Kulia kabisa ni Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed
UN /Manuel Elias

UNGA 77 yafunga pazia, Rais wa UNGA78 ala kiapo

Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umekunja jamvi asubuhi ya tarehe 5 Septemba 2023, jijini New York, Marekani kwa Rais wa mkutano huo anayemaliza muda wake Csaba Kőrösi akisisitiza kuwa licha ya mikingamo ya kijiografia, ushirikiano baina ya nchi haukwepeki.