Pamoja na jitihada zinazofanyika amani kwetu bado ni kitendawili: Rais Al-Alimi
Pamoja na jitihada zinazofanyika amani kwetu bado ni kitendawili: Rais Al-Alimi
Rais Rashad Mohammed Al-Alimi wa baraza la Urais la Yemen alihutubia katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA78 hii leo amesema amani bado ni kitendawili kigumu katika nchi yake licha ya juhudi kubwa za kikanda na kimataifa zinazofanyika kuurejesha utulivu.
"Tumelazimika kujenga upya taasisi zetu, ilibidi tuanzishe tena Baraza la uongozi wa rais kwa kuzingatia ushirikiano wa kujenga amani na kumaliza vita." Amesema Al-Alimi na kuongeza kuwa, "Tunajua kwamba tunahitaji ushirikiano ili kujenga nchi yetu, ili kufikia mustakabali bora."
Hakuna tunachoweza kuwashawishi Houthi
Bwana Alami anaamini muda unawatupa mkono linapokuja suala la wanamgambo wa Houthi "leo siamini kuwa tuna muda wa kutosha, au tuna maelewano ya kutosha ya kufanya ili kuwashawishi wanamgambo wa Houthi kubadili misimamo yao. Tunaweza hata kutabiri dhamira zao kwa miongo kadhaa ijayo. Tukifanya hivyo, mbinu hii itawarudisha watu wa Yemen kwenye zama za ujinga na ukandamizaji.”
Amehitimisha hotuba yake kwa kutoa tahadhari kwamba hatua Madhubuti zisipoichukuliwa kuna hatari kwamba “ Nchi yetu inaweza hata kuwa kitovu cha kusafirisha ugaidi na kuanzisha mzozo wa kikanda na kimataifa ambao hauwezi kuzuilika.”
Kusikiliza hotuba yake yote bofya hapa.