Urusi kutumia chakula na nishati kama silaha ni madhara kwa nchi zote: Zelenskyy
Urusi kutumia chakula na nishati kama silaha ni madhara kwa nchi zote: Zelenskyy
Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine leo amewaambia viongozi wa dunia katika mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba “pamoja na tishio lake la nyuklia linaloendelea, Urusi pia inatumia silaha muhimu kama vile soko la kimataifa la chakula na nishati na inazitumia sio tu dhidi ya nchi yetu, lakini nchi zenu wote pia."
Ameendelea kusema kwamba tangu kuanza kwa vita, bandari za Ukraine katika bahari ya Nyeusi na Azov zilizuiliwa na Urusi na bandari zake kwenye Mto Danube zikilengwa na ndege zisizo na rubani au drones na makombora.
"Ni jaribio la wazi la Urusi la kutumia uhaba wa chakula kwenye soko la kimataifa kama silaha, ili kubadilishana na kutambuliwa kwa baadhi ya maeneo yaliyotekwa."
Rais huyo wa Ukraine amesema athari za silaha hizo zinaonekana kuanzia Afrika hadi Kusini-Mashariki mwa Asia.
"Nyuklia sio tena jambo la kutisha zaidi kwa sasa. Uharibifu mkubwa unaendelea kushika kasi. Mvamizi huyo anatumia vitu vingi kama silaha, vitu ambavyo vinatumiwa sio tu dhidi ya nchi yetu lakini pia yako," amesema na kuongeza kuwa "Kuna mikataba mingi dhidi ya silaha lakini hakuna hata mmoja dhidi ya silaha ya usambazaji wa chakula na nishati duniani."
Bofya hapa kwa tarifa zaidi za hotuba yake.