Chuja:

Makala Maalum

Mpishi wa shule
© WFP/Emily Fredenberg and Fredrik Lerneryd

WFP na wakfu wa Rockefeller wazindua mradi wa kuimarisha mlo shuleni

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, linakaribisha msaada wa dola milioni 10.7 kutoka kwa wakfu wa Rockefeller ili kuwasaidia mamilioni ya watoto walio katika mazingira magumu kupata fursa ya chakula chenye lishe bora kupitia programu za mlo shuleni nchini Benin, Ghana, Honduras na India. Mradi huo wa miaka miwili na nusu unalenga katika kujumuisha vyakula vilivyoimarishwa kwenye milo ya shuleni pamoja na kuchagiza chakula chenye lishe zaidi katika programu zote. 

Pichani, Isatou, Mariama na Fatoumatta hawalazimiki tena kutoenda shule wakati wa hedhi baada ya UNFPA kusaidia uzalishaji na mgao wa bure wa taulo za kike zitumikazo tena na tena wa ajili ya shule ikiwemo shule yao ya viziwi mjini Banjul, Gambia.
UNFPA Gambia

Sababu 8 za matumaini kwa mwaka mpya 2023

 “Kama kuna vifo, hiyo ndio itakuwa habari ya juu,” ni msemo wa siku nyingi katika vyumba vya habari, ukiangazia vile ambavyo vyombo vya habari vinapatia kipaumbele habari za majanga. Ukitazama nyuma mwaka 2022, uligubikwa na vichwa vya habari vyenye kiza, matangazo ya kutia hofu na tabiri chungu za siku zijazo. Si kila mtu ameweza kuona maendeleo yaliyopatikana, ikiwemo kusongesha ubunifu, haki, uwiano na usawa duniani kote.

Paulina Ajello mfanyakazi wa WHO kitengo cha mawasiliano na ushirikishaji jamii akizungumza na wanajamii waelimishaji kuhusu Ebola.
Picha: WHO_Uganda/PhilipKairu

Jiji la Kampala laendesha kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Ebola

Wakati huu ambapo hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyesajiliwa katika mji mkuu wa Uganda tangu tarehe 14 Novemba, 2022 mamlaka ya afya ya Mji Mkuu wa Kampala kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya nchi hiyo hivi karibuni ilifanya kampeni ya siku saba kuelimisha umma ili kudumisha umakini wa watu na hatimaye kusaidia kumaliza mlipuko wa ugonjwa huo hatari duniani.