Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rambaza Wavuti mpya wa Habari za UN

Kunani?

Wavuti wa Radio ya Umoja wa Mataifa unafungwa rasmi mwishoni mwa mwezi Januari 2018. Nafasi yake itachukuliwa na ukurasa mpya ambao tuna imani utawapatia wasikilizaji na washirika katika vituo mbali mbali vya radio duniani, taarifa bora zaidi katika muundo tofauti.

Idara ya Habari kwa Umma ya Umoja wa Mataifa inayo furaha kuzindua wavuti huo ambamo kwao utapata taarifa katika mifumo yote. Mabadiliko haya kutoka Radio ya Umoja wa Mataifa hadi Habari za UN ni matokeo ya tafiti za kina kuhusu matumizi na mahitaji ya hadhira yetu.

Kwa nini?

Tunataka Habari za UN iwe mlango unaokuwezesha kurambaza katika kurasa za Umoja wa Mataifa kwa urahisi zaidi, iwe ni masuala ya ulinzi wa amani, maendeleo au haki za binadamu- wakimbizi au silaha za nyuklia- na simulizi nyingi zaidi za kiutu nyuma ya pazia la habari hizo.Halikdhalika tunataka uweze kupata kwa urahisi zaidi, habari, makala na majarida kuhusu simulizi za kibinadamu zikiwa zimejumuishiwa sauti, video, picha, maneno kwa uzoefu zaidi wa habari za kisasa.

Nani?

Kutoka chumba chetu cha habari kwenye makao makuu ya UN, jopo letu la uhariri kila siku linaandaa habari katika lugha nane kwa kuzingatia matukio ya siku, kampeni, mikakati mikubwa na taarifa nyingine kutoka kwa washirika wa UN. Waandaaji wetu wa vipindi wanahoji wafanyakazi wa UN kutoka mashinani au ndani ya studio, halikadhalika wananchi ambao tunawahudumia, kila siku na popote duniani.

Vipi?

Unaweza kupata habari kupitia jukwaa letu jipya yaani wavuti wetu, lakini pia unaweza kujisajili kwa barua pepe ili kujulishwa punde tu Habari mpya ya UN au Sauti inapopakiwa. Unaweza pia kupakua Apu zetu za UN News au Audio Now kupitia iOS na Android – Lakini pia kupitia majukwaa yetu ya kijamii. Unaweza pia kuhifadhi habari kwenye kabrasha na kuisoma baadaye, ukaunda msururu wako wa kile unachotaka kusikiliza na pia ukabadilishana na wengine habari hizo kwa njia mbalimbali.

Tafadhali tumia huduma zetu.

Tutafurahi sana ukitumia habari hizi kama zilizvyo au ukaongeza au kupunguza bila kupoteza maana. Hata eleza bayana kuwa ni mali ya Habari za UN. Na zaidi ya yote zingatia hakimiliki kwenye matumizi ya picha, sauti na video. Iwapo una wasiwasi wasiliana nasi kupitia unnews@un.org

Twasubiria kwa hamu kusikia kutoka kwako.