Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 SEPTEMBA 2023

18 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tuanaangazia malengo ya maendeleo endelevu na tutasalia hapa makao makuu ya umoja wa Mataifa kwenye Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo hayo.

  1. Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, limefungua pazia leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuja na azimio la kisiasa la kuhakikissha wanayanusuru malengo hayo ambayo mengi yanakwenda mrama kwani ni asilimia 15 pekee kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndio yametimizwa huku ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufikia mwaka 2030 ukomo wa utimizaji wa malengo hayo.
  2. Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030.   
  3. Katika makala Thelma Mwadzaya amefuatilia na kukuletea makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs.
  4. Mashinani tunasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani kusikia kile ambacho vijana wanataka kifanyike ili malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaweze kufanikiwa, lakini kwanza ni makala nampisha Thelma Mwadzaya na makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'18"