SOFEPADI yarejeshea matumaini waathirika wa vita Mashariki mwa DRC
Mmoja wa washindi wa tuzo ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2023 ni Julienne Lusenge, muasisi na Mkurugenzi wa shirika la kiraia la SOFEPADI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Msingi wa ushindi wake ni miradi inayotekeleza yenye lengo la kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia na watu walioathiriwa na mapigano mashariki mwa taifa hilo. Moja ya miradi hiyo ni Tujenge Amani Leo.
Habari Zaidi katika picha
Pagination
- Page 1
- Next page