Ukuaji wa Kiuchumi

Zanzibar inasonga kuwawezesha wanawake vijijini: Fatma Bilal

Serikali ya Zanzibar imekuwa mfano wa kuigwa katika suala la uwezeshaji wanawake vijijini kujikwamua na umasikini kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo kama ilivyo  katika ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. 

Kuondoka kundi la LDCs ni faida zaidi kuliko hasara- Gay

Hii leo kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu sera za maendeleo, CDP inatangaza nchi ambazo zimefanikiwa kutoka katika kundi la nchi zilizo katika harakati za kujikwamua kiuchumi, LDCs.

FAO yazindua app ya kukabiliana na viwavijeshi Afrika

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO , leo limezindua huduma ya kimtandao yaani app, itakayosaidia wakulima  barani Afrika kugundua mapema na   kupambana na tatizo la viwavijeshi katika mimea.

Azma ya maendeleo ya viwanda Tanzania imetuvutia- UNIDO

Tanzania ya viwanda ni jambo ambalo limevutia wengi ikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maeneleo ya viwanda UNIDO. Sasa UNIDO imechukua hatua kuona ndoto hiyo ya Tanzania inatimia.

Pengo la ajira kati ya wanawake na wanaume lingali kubwa- ILO

Ripoti mpya ya shirila la kazi duniani ILO imesema japo hatua zimepigwa katika harakati za usawa wa kijinsia, bado kuna pengo kubwa kwenye soko la ajira kati ya wanawake na wanaume.

Bei ya chakula imepanda kwa aslimia 1.1 Februari :FAO

Ripoti ya Februari ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO imebaini ongezeko la asilimia 1.1 la bei ya nafaka duniani Ikilinganishwa na mwezi Januari mwaka huu.

Misaada ya kujikwamua ni muhimu zaidi kwa wakimbizi Chad

Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na  usaidizi wa majanga, OCHA, Ursula Mueller amehitimisha ziara yake huko Chad iliyolenga kujionea hali halisi ya athari za mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram. 

Mabadiliko ya tabianchi yataathiri uzalishaji wa mazao kusini mwa Afrika

Ripoti kutoka shirika la chakula na kilimo duniani FAO, imesema ongezeko la joto na ukosefu wa nvua kusini mwa bara la Afrika vitaathiri  sana sekta ya kilimo mwaka huu, na kufanya  usalishajji wa mazao kupungua kwa kiasi kikubwa.

Chad taifa la kwanza Afrika kujiunga na mkataba wa maji:UNICE

Chad imekuwa taifa la kwanza barani Afrika nje ya kanda ya Ulaya kuridhia mkataba wa ulinzi na matumizi ya mipango ya rasilimali ya maji na maziwa ya kimataifa unaosimamiwa na tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ulaya (UNECE).

Vijana lazima wawezeshwe ili kufanikisha SDGs: UN

Mataifa yanayoendelea yameshauriwa, miongoni mwa mambo mengine, kuwawezesha vijana na  pia kuhakikisha usawa wa  kijinsia ili kufanikisha  malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.