Neno La Wiki

Neno la Wiki- "Wame"

Leo katika Neno la Wiki tunakwenda kwa mtaalam wetu wa kiswahili juma hili ambaye ni Mwanahija Ali Juma katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar , BAKIZA anafafanua matumizi ya neno “WAME” katika sentensi yenye nomino mbili.

 

 

 

 

 

Sauti -
1'12"

Neno la wiki-MSUMBI

Mchambuzi wetu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania , BAKITA ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi anafafanua maana ya neno "MSUMBI"

 

Sauti -
1'

Neno la wiki-Baba alimpiga binti yake kwa kuwa alilewa

Na leo katika neno la wiki inaelezewa sentensi ambayo imejadiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii na kwingine isemayo, baba alimpiga binti yake kwa kuwa alilewa.

Sauti -
58"

Neno la Wiki- Afkani

Hii leo katika NENO LA WIKI, Mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo  anatufafanulia maana ya neno Afkani.

Sauti -
41"

Neno la Wiki- Kafala

Na sasa ni neno la wiki ambapo Onni Sigalla,  Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anachambua maana ya neno Kafala . Bwana Sigalla anafafanua maana mbili za neno hilo na akisisitiza kwamba ni tofauti na Kafara.

Sauti -
45"

Neno la Wiki- "Ukikaa na Simba, vaa ngozi ya mamba"

Katika Neno la Wiki hii leo tunachambua methali isemayo, "Ukikaa na Simba, vaa ngozi ya mamba." Mchambuzi wetu ni Ken Walibora, mwanariwaya na na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA. Fuatana naye mlumbi huyu wa lugha ya Kiswahili.

Sauti -
42"

Neno la Wiki: Mchirizi na Mtaro

Katika neno la wiki hii leo tunabisha hodi, Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA ambako mchambuzi wetu  Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo anafafanua maana ya maneno MTARO na MCHIRIZI.

 

Sauti -
49"

Neno la Wiki: Tembe, Mtetea, Koo, Kiweto, Kipora

Katika neno la wiki hii leo mchambuzi wetu Aida Mutenyo kutoka Uganda anachambua majina mbalimbaliya Kuku. Kuna Tembe, Mtetea, Koo, Kiweto na Kipora. Je wafahamu tofauti zake? Ungana na Bi. Mutenyo ambaye ni Mwenyekiti wa Idara za Kiswahili za Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki.

Sauti -
1'11"

Neno la Wiki-NASIHA

Na sasa ni muda wa kujifunza Kiswahili na leo mchambuzi wetu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania , BAKITA ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi anafafanua maana ya neno "NASIHA"

Sauti -
41"

Neno la Wiki- Komangu

Na sasa ni neno la wiki ambapo Onni Sigalla,  Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anachambua maana ya neno Komangu. Je neno hili lina maana gani, ungana naye kwa undani zaidi.

Sauti -
47"