Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA78

MKUTANO WA 78 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA78

Jukwaa  limeandaliwa kwa ajili ya mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati ulimwengu ukiendelea kukabiliwa na mdororo wa kijamii na kiuchumi kutokana na Covid 19 na athari zinazoendelea za vita nchini Ukraine, mjadala utafanyika kikamlifu ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019, na viongozi wa ulimwengu wakielekea NY kuwasilisha kauli zao katika Ukumbi mashuhuri. 

Hapa, Habari za UN inakupa kiti cha mstari wa mbele katika shughuli zote. Katika simu yako ya mkononi au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapofafanua hatua dhidi ya changamoto kubwa zaidi duniani na kushiriki katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hatua kabambe ya kumaliza janga la tabianchi, na vikao vitatu vya ngazi ya juu visivyo na kifani kuhusu afya: maandalizi dhidi ya majangahuduma ya afya kwa wote; na mapambano ya kimataifa dhidi ya kifua kikuu

Tutembelee kwenye majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

Twitter: twitter.com/HabarizaUN

Youtube: https://www.youtube.com/@UNNewsKiswahili 

UN News

Tanzania tumepiga hatua kubwa kupambana na kifua kikuu: Waziri Ummy Mwalimu

Kifua kikuu au TB ni moja ya changamoto kubwa za kiafya duniani na janga ni kubwa zaidi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO duniani kote, TB ni sababu ya 13 inayoongoza kwa vifo na ya pili muuaji wa magonjwa ya kuambukiza baada ya COVID-19 ikiwa juu ya VVU na Ukimwi. Shirika hilo linakadiria kwamba mwaka 2021, takriban watu milioni 10.6 waliugua kifua kikuu kote duniani wakiwemo wanaume milioni sita, wanawake milioni 3.4 na watoto milioni 1.2.

Sauti
3'39"