Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCTAD/UNECA: Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.

Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.
UNCTAD
Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.

UNCTAD/UNECA: Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia upatu lengo namba tano la Malengo Endelevu ya Umoja huo linalohimiza usawa kwa wote katika nyanja zote ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo ili kuelewa jinsi biashara inavyoathiri wanaume na wanawake ni muhimu kuunda sera za biashara zinazojumuisha zaidi na zenye usawa ambazo zinakuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wote,hii inahitaji takwimu nzuri za kitaifa kuhusu jinsia katika biashara.

Kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi ya Afrika UNECA, Kenya inaunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara. 

Soundcloud

Hatua hii ya kuunda viashiria vipya inakuja wakati huu ambapo haja ya takwimu za biashara kijinsia inazidi kuwa kubwa huku serikali ikijitahidi kubuni sera za biashara zinazozingatia jinsia.

Kenya ilifanya majaribio mbinu za UNCTAD na kukusanya viashiria vipya vya majaribio, vilivyotofautishwa kijinsia vinavyopima ajira, mishahara na umiliki wa biashara katika sekta ya biashara, kama navyoeleza Stanley Wambura kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu nchini Kenya, anasema  “Sasa, mradi wa jinsia na takwimu ni muhimu sana kwetu nchini Kenya, kwa maana ya kwamba utakapoendeshwa kikamilifu, tutaweza kupata takwimu ambazo zitatusaidia kuweza kufanya ufuatiliaji wa lengo namba tano la SDG”

Stanley anaongeza kwa kusisitiza kwamba, "Ni muhimu sana kwetu, pia kuna sera nyingine za kitaifa haswa za usawa wa kijinsia, kwamba takwimu hizi zitaelekeza jinsi tunavyopanga, jinsi tunavyounda sera na kusimamia sera na mwishowe, tutaweza kushambulia hadhi ya usawa nchini Kenya”.

Je, ni yapi matokeo ya kuvutia ya mradi huu nchini Kenya? 

Dkt. Francis Omondi ambaye ni Mshauri wa Kitaifa wa UNECA nchini Kenya anasema,“Ugunduzi wa kustaajabisha uliotokana na uchunguzi wa majaribio ambao ulifanywa nchini Kenya umegundua ya kwamba umiliki wa biashara kwakuzingatia jinsia ulibainisha idadi ya wafanyakazi wa kiume na wa kike, pamoja na mishahara wafanyakazi wa kiume na wa kike. Kwa hiyo tumegundua ya kuwa makampuni ya biashara yaliyo na viongozi wa juu wa kiume pekee, wafanyakazi wake wengi zaidi ni wakiume; kuliko wafanyakazi wa kike. Kwa upande mwingine ambapo kulikuwa na mchanganyiko katika umiliki wa makampuni ya biashara, ajira kwa wanaume na wanawake ilikuwa karibu sawa. Lakini linapokuja suala la pengo la mishahara, inaonekana kwamba kama vile makampuni ya wanawake pekee yaliajiri wanaume zaidi kuliko wanawake, yalielekea kuwalipa wafanyakazi wao wa kike zaidi ya wafanyakazi wa kiume”.

Cynthia Chelimo,Afisa kutoka Idara ya biashara ya serikali ya Kenya.
UNCTAD
Cynthia Chelimo,Afisa kutoka Idara ya biashara ya serikali ya Kenya.

Cynthia Chelimo kutoka Idara ya biashara ya serikali ya Kenya anaongeza kuwa “Mafunzo ambayo tumejifunza kutoka kwa mradi huu wa majaribio ni kwamba takwimu iliyogawanywa kwa jinsia ni muhimu sana katika suala la kuunda sera nchini Kenya, tutawawezesha wanawake na wataweza kuchangia zaidi uchumi wa Kenya”.

Ama hakika usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara ni muhimu ili kupunguza ama kuondoa kabisa pengo la mshahara baina ya wanawake na wanaume na pia kuhakikisha makampuni yana viongozi wakike na wakiume katika nafasi za juu za uongozi.