Wazazi nchini Tanzania wameupokea vizuri mradi unaotekelezwa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, la masuala ya idadi ya UNFPA na la wanawake UN Women, ambao unalenga kuwawezesha wasichana kupitia elimu. Baada ya jana kuwaangazia wasichana wanufaika wa mradi huu, leo, Ahimidiwe Olotu ametuandalia sehemu ya pili inayoangazia wazazi na wanajamii kwa ujumla.