Fahamu mambo 5 muhimu kutoka hotuba ya Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini kwa UNGA78
Fahamu mambo 5 muhimu kutoka hotuba ya Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini kwa UNGA78
Afrika haiko tayari kuendelea kubeba gharama za mapinduzi ya viwanda na maendeleo ya nchi tajiri, ni moja ya kauli kutoka hotuba ya Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akihutubia mjadala mkuu wa UNGA78 jijini New York, Marekani.
Mosi: Baada ya kumalizika utumwa na ukoloni sasa basi
Karne kadhaa baada ya kumalizika kwa biashara ya utumwa, miongo kadhaa baada ya kumalizika kwa ukoloni uliopora rasilimali za Afrika, wananchi wa bara letu wanalipa gharama ya mapinduzi ya viwanda na maendeleo ya nchi tajiri, gharama ambayo katu hawako tayari tena kulipa.
Pili: Nchi tajiri zitekeleza ahadi kupunguza hewa ya ukaa
Rais Ramaphosa amesihi viongozi wa dunia waongeze kasi ya kupunguza hewa ya ukaa huku wakizingatia usawa na ustawi wa pamoja.
Tatu: Rasilimali za Afrika zinufaishe waafrika
Jambo lingine alilozungumzia ni rasilimali zilizo barani Afrika akisema utajiri wa Afrika ni mali ya waafrika, madini yaliyomo kwenye ardhi lazima mwisho wake yawanufaishe waafrika.
Nne: Ajabu matrilioni kuelekezwa vitani mamilioni wana njaa
Wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2022 watu milioni 783 walikabiliwa na njaa duniani kote, Rais Ramaphosa anasema ni kosa kubwa mno la jamii hii ya kimataifa kuwa tunaweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha, ni kwamba matrilioni ya fedha kwenye vita, lakini hatuwezi kusaidia hatua zinazopaswa kuchukuliwa kukidhi mahitaji ya mabilioni ya watu, wenye njaa, huduma za afya, kuwezesha wanawake na kuhakikisha kuna maendeleo katika nchi zilizo hatarini.
Tano: Nchi tajiri timizeni ahadi
Nchi tajiri zitimize ahdi walizotoa za ufadhili “inatia hofu nchi hizi Tajiri zimeshindwa kutimiza ahadi ya kuchangia dola bilioni 100 kila mwaka kwa nchi zinazoendelea kutekeleza miradi ya hatua kwa tabianchi.
Tazama hapa hotuba ya Rais Ramaphosa