Makala

Wakulima Bolivia waanza kufuata utaalam wa kijadi kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Wakati viongozi wa ndunia wakiendelea kukuna vichwa mjini Katowice nchini Poland kusaka dawa mujarabu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye mkutano wa COP24 hadi Disemba 14, jinamizi hilo limeendelea kuziathiri jamii mbalimbali duniani.  Nchini Bolivia, takriban asilimia 40 ya watu wa

Sauti -
3'17"

Utamaduni wa jamii yako ni haki  yako, lasema tamko la haki za binadamu la UN

Katika mwendelezo wa uchambuzi wa ibara kwa ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo tunamulika ibara ya 27 inayosema kuwa kila mtu ana haki ya kushiriki na kunufaika na tamaduni, sanaa na sayansi ya jamii yake.

Sauti -
2'2"

Mkimbizi bila elimu ni sawa na mti bila matunda:Mkimbizi Rachel

Elimu kwa mkimbizi ni muhimu sana, kwani bila elimu huwezi fanya chochote , iwe ni kwa upande wa ajira au hata ujasiriliamali, unakuwa sawa na mti usiozaa matunda ambao huonekana kutokuwa na faida yoyote.

Sauti -
3'32"

Ibara ya 24

Mapumziko na burudani ikiwemo kuwa na muda wenye ukomo wa kufanya kazi na pia kupatiwa likizo yenye malipo ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa  Ibara ya 24 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwezi huu. Lakini je haki hii ya msingi inatekelezwa vipi?

Sauti -
2'11"

Hali ya baadhi ya wafanyakazi ughaibuni inasikitisha- Emma Mbura

Ibara ya 23 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa inasema kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuchagua kazi anayoifanya, kufanya kazi katika mazingira salama na ulinzi dhidi ya ukosefu wa ajira.

Sauti -
5'14"

Jamaica yafurahi muziki wake wa mtindo wa Reggae kutambuliwa na UNESCO

Muziki mbali na kuelimisha, kufahamisha, kuliwaza ama kuburudisha lakini pia kwa upande mwingine ni tunu inayotumika kutambulisha jamii ya eneo fulani kwa wakati fulani. Kupitia muziki, jamii kutoka upande mmoja inaweza kufahamu utambulisho wa mwingine na imefika wakati hata jamii moja kuiga tama

Sauti -
1'27"

Kubadili mifumo ndio muarobaini wa haki za huduma za jamii Tanzania: Dkt.Bisimba

Nchini Tanzania ingawa katika katiba  imeaainishwa haki za huduma za jamii kwa wote, mifumo iliyopo inafanya kuwa changamoto kubwa ya utekelezaji wa haki hizo. Hayo yamesemwa na Dkt.Helen Kijo Bisimba mwanaharakati wa muda mrefu wa haki za binadamu nchini humo.

Sauti -
5'29"

Katu mtu asilazimishwe kujiunga na chama hata ndani ya familia- Wakili Komba

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka  huu linatimiza miaka 70 tangu kuasisiwa lina ibara 30 ambazo ni msingi wa haki za binadamu kote duniani.

Sauti -
4'18"

Anasemekana kuwa mwanamke wa kwanza wa kanda ya Afrika mashariki na kati kupata shahada ya Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza mwaka wa 1954.

Wakati  harakati za siku 16 za kuhamasisha kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake zikiwa zinaendelea, leo tuko nchini Uganda kusikia mchango wa mama mmoja ambae sasa ni marehemu lakini alikuwa mpigania haki za wanawake nchini humo.

Sauti -
3'12"

Nuru yaonekana katika juhudi za kulinda maeneo oevu, Uganda

Ulinzi wa mazingira umekuwa ukipigiwa upatu na Umoja wa Mataifa kama moja wa juhudi za kuona dunia yetu haihatarishwi na majanga yatokanayo  na uharibifu wa mazingira.

Sauti -
3'47"