Afya

Wafanyakazi wa ndani bado wanalilia maslahi yao: ILO

Licha ya muongo mmoja wa uwepo wa mkataba wa kimataifa wa haki za wafanyakazi wa ndani,  bado kada hiyo inaendelea kupigania usawa na mazingira bora ya kazi huku janga la ugonjwa wa Corona au COVID19 likionesha dhahiri udhaifu uliopo katika kada hiyo.

Watoto 33,000 hatarini kufa nchini Ethiopia- UNICEF

Takriban watoto 33,000 katika eneo ambalo halifikiki la Tigray nchini Ethiopia wana utapiamlo mkali na wanakabiliwa na vifo iwapo msaada wa haraka hautapatikana, imesema taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Henrietta Fore iliyotolewa leo jijini New York, Marekani. 
 
 

COVID-19 yasababisha kupungua kwa kiwango cha uchangiaji damu Afrika- WHO 

Leo ni siku ya kuchangia damu duniani ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani,  WHO mwaka huu siku hiyo inajikita na vijana na mchango wao katika kuokoa maisha kwa kujitolea damu. Kauli mbiu ikiwa“Toa damu na kuhakikisha dunia inaendelea kuishi”.  

Asanteni viongozi G-7 kwa ahadi ya kugawa chanjo za COVID-19- UNICEF

Uamuzi wa kundi la nchi 7, G7 zenye viwanda zaidi duniani wa kutoa chanjo angalau milioni 870 dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 umeungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.

Chanjo zinapaswa kuzingatiwa kama "bidhaa za umma ulimwenguni" - Guterres 

Akiongea kupitia video huko London, Uingereza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema hakuna njia nyingine ya kushinda virusi vinavyoenea katika nchi zinazoendelea "kama moto wa nyikani" na hatari za kubadilika, isipokuwa kwa njia ya usawa, chanjo kwa watu wengi, na kuongeza kuwa chanjo zinahitajika "kupatikana na za bei nafuu kwa wote ” 

COVID-19 yashika kasi Afrika, chanjo ni haba, Uganda hali si  hali

Idadi ya wagonjwa wa Corona au COVID-19 inavyoendelea kuongezeka kwa wiki tatu mfululizo barani Afrika huku chanjo ikisalia kuwa haba, mataifa 47 kati ya 54 barani humo yanaelekea kutofikia lengo la kutokuwa yamepatia chanjo angalau asilimia 10 ya wananchi wake ifikapo mwezi Septemba mwaka huu. 

Usugu zaidi wa dawa dhidi ya E.Coli na magonjwa ya zinaa waripotiwa

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kuhusu ufuatiliaji wa maambukizi ya magonjwa katika maabara na matokeo ya usugu wa dawa dhidi ya vijiumbe maradhi, GLASS, inatia matumaini kuwa hivi sasa maabara nyingi zinafanya uchunguzi wa usugu huo na hivyo kutoa fursa ya utafiti na kudhibiti usugu wa dawa.
 

UKIMWI Tanzania hivi sasa siyo tena hukumu ya kifo- Rais Samia

Tanzania imesema inaunga mkono mshikamano wa kimataifa wa kutokomeza Ukimwi duniani, kauli iliyotolewa leo na Rais wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI ulioanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao na ukumbini.
 

Je chakula unachokula ni kisafi na hautopata magonjwa? 

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ya usalama wa chakula duniani, ambapo mashirika ya  Umoja wa Mataifa lile la afya ulimwenguni -WHO na la Kilimo na chakula FAO yametoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kuhakikisha chakula kinacholiwa ni salama na kulifanya suala la usalama wa chakula kwa umma ni ajenda ya wote, ili kupunguza magonjwa yanayosababishwa na chakula kisicho bora na salama. 

WHO yatiwa hofu na awamu nyingine ya COVID-19 Afrika 

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO limeonya kuwa hospitali barani Afrika ziko hatarini kuelewa na wagonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 wakati huu ambapo upelekaji wa chanjo barani humo unasuasua huku majira ya baridi yakitishia kusambaa kwa kasi kwa virusi hivyo.