Sauti Mpya

22 Machi, 2018

Katika Jarida hii leo, Siraj Kalyango anaangazia siku ya Maji tukimulika wakazi wa jamii ya warendile huko Marsabit nchini Kenya. Vijana wakutana New York, Marekani kujifunza muundo wa UN. Sudan Kusini wakimbizi wa ndani waanza kurejea wakimwomba mola awageukie.

Sauti -
10'20"

Maji safi bado mkwamo kwa warendile huko Marsabit

Leo ni siku ya maji duniani ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo uhifadhi wa mazingira halisi ya eneo husika kama njia moja ya kukabiliana na uhaba wa maji duniani.

Sauti -
1'31"

Mchango wa vijana kwa suluhu ya wakimbizi waweza kufaa

Vijana wanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kusaka suluhu ya changamoto zinazowakabili wakimbizi na hasa vijana wenzao. Hayo yamesemwa na baadhi ya vijana wanaohudhuria vikao vya mfano wa Umoja wa Mataifa (Model UN) vinavyohitimishwa leo mjini New York Marekani.

Sauti -
1'25"

Eh Mola turejeshee furaha yetu- Wakimbizi

Nchini Sudan Kusini msimu wa mvua ukitarajiwa kuanza, baadhi ya wakimbizi wa ndani na hata wale waliokimbilia nchi za jirani wameamua kurudi nyumbani angalau kuendelea na maisha yao. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Sauti -
1'22"

Pepo za monsuni zatishia uhai wa warohingya

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Cate Blanchett ametaka hatua za dharura kulinda na kusaidia wakimbizi wa Rohingya walioko Bangladesh, wakati huu ambapo pepo za monsuni zinatishia usalama wao.

Sauti -
1'30"

Vijana wanaotumia mihadarati wasaidiwe badala ya kutiwa mbaroni

Matukio ya matumizi ya kupindukia ya madawa ya kulevya yametawala katika nchini zilizoko Mashariki mwa Afrika. Serikali pamoja  mashirika ya kibinadamu wamekuwa bega kwa bega kupambana na zahma hiyo inayoangamiza kizazi cha leo hususani vijana.

Sauti -
3'46"

Malengo ya SDG’s yatamalaki siku ya ushairi duniani

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya ushairi duniani hii leo, siku iliyotengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO  kwa lengo la kuchagiza usomaji, uandishi, uchapishaji na ufundishaji wa ushairi, mwaka huu imetoa msukomo katika kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu SDG’s. Tanzania haikusalia nyuma. 

Sauti -
1'24"

Azimio la Kigali kuhusu eneo la biashara huru barani Afrika latiwa saini

Nchi za Afrika zimeridhia azimio la Kigali kuhusu eneo la biashara huru barani himo na hivyo kuhitimisha harakati za miaka zaidi ya 40 tangu tamko la utekelezaji la Lagos la kutaka kuwa na eneo kama hilo. 

Sauti -
1'21"

21 Machi 2018

Katika jarida la leo tunakuletea habari njema ya maridhiano ya azimio la Kigali kuhusu eneo la biashara huru barani Africa.  Pia tukiadhimisha siku ya ushairi duniani hii leo, shairi la Love Mcharo  linaghaniwa na Nasir Ibrahim kutoka Tanzania katika harakati za kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.

Sauti -
9'54"

Kama umasikini ungekuwa na sura, basi ni ya mwanamke wa kijijini: IFAD

Watu bilioni 1.7 wanaishi vijijini kote duniani huku zaidi ya asilimia 40 ya nguvu kazi yao katika kilimo ni wanawake  ambao  wakiilisha na kuindeleza jamii lakini wanasalia kuwa ndio masikini wakubwa.

Sauti -
1'23"