Amani na Usalama

Tushughulikie kiini cha udhalilishaji wa kijinsia: Guterres

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia katika maeneo yenye mizozo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antoni Guterres amdewataka waokozi kuzingatia hali na mahitaji ya waathiriwa wa udhalilisha wakati wakiwa wanafanya kazi ya kuzuia na kumaliza kabisa janga hilo la udhalilishaji ambalo ni kosa la inai.

UNHCR yaitisha mkutano na wadau kuijadili suluhu ya Venezuela

Venezuela, moja kati ya Mataifa ambayo wananchi wake wanalikimbia kwa wingi takwimu kwenda kuomba hifadhi mataifa mengine ambapo takwimu za hivi karibuni zinaonesha takribani robo ya wananchi wake wamekimbia hali ambayo imeshafanya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano hii leo kutafuta suluhu ya kudumu. Tuungane na Leah Mushi kwa undani wa taarifa hii

Mwendesha Mashtaka Mkuu Mpya wa ICC aapishwa Rasmi

“Naapa kwamba nitatekeleza majukumu yangu kwa Mamlaka yangu ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Kamosa ya Jinai kwa heshima, uaminifu, bila upendeleo na kwa dhamiri, nitaheshimu usiri kwenye kufanya uchunguzi na kuendesha mashtaka” kiapo cha Mkuu mpya wa ICC

 

Kauli za chuki zinaongezeka DRC, hatua zichukuliwe:Keita 

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Bintou Keita, amelaani vikali kuenea kwa ujumbe unaochochea chuki, vurugu na uhasama baina ya jamii kwenye majimbo kadhaa ya nchi hiyo. 

Maelfu ya waliotawanywa na volkano DRC wahitaji msaada wa haraka:UNHCR

Mamia kwa maelfu ya watu waliotawanywa na mlipuko wa volcano wa mlima Nyiragongo Masharki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, sasa wanahitaji msaada wa haraka katika maeneo walikokimbilia na kupata hifadhi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Flora Nducha anasimulia zaidi 

UN na zoezi la kijeshi kuimarisha vikosi vya Lebanon, kulikoni?

Huko nchini Lebanon, ujumbe wa kikosi cha mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, umefanya mazoezi ya siku tano pamoja na vikosi vya usalama vya taifa hilo, LAF kama sehemu ya kujengea uwezo jeshi hilo la kitaifa kwa ajli ya kuimarisha amani na usalama.
 

UN imelaani vikali shambulio la kutisha hospitali nchini Syria

 Maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali shambulio baya lililofanyika katika hospitali nchini Syria mwishoni mwa wiki na kusisitiza haja ya uwajibikaji kwa uhalifu uliofanywa katika vita vya miaka kumi vya nchi hiyo. 
 

Watoto 33,000 hatarini kufa nchini Ethiopia- UNICEF

Takriban watoto 33,000 katika eneo ambalo halifikiki la Tigray nchini Ethiopia wana utapiamlo mkali na wanakabiliwa na vifo iwapo msaada wa haraka hautapatikana, imesema taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Henrietta Fore iliyotolewa leo jijini New York, Marekani. 
 
 

Ghasia Cabo Delgado, wanaokimbilia Tanzania waendelea kurejeshwa

Nchini Msumbiji katika mji wa pwani wa Palma jimboni Cabo Delgado bado wananchi wanaripoti kusikia milio ya risasi kila uchao, nyumba zao zikitiwa moto na hivyo kulazimika kukimbia maeneo mengine ndani ya nchi yao au hata kuvuka mpaka na kuingia Tanzania, hali inayoendelea kutia hofu kubwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kuhusu usalama wao.
 

Watu 350,000 wanakabiliwa na baa la njaa Tigray, msaada wahitajika haraka kunusuru maisha:UN

Takwimu mpya na za kusikitisha zilizotolewa leo zimethibitisha ukubwa wa dharura ya njaa inayolighubika jimbo la Tigray nchini Ethiopia ambako watu milioni 4 wanakabiliwa na njaa kali na wengine 350,000 tayari wanakubwa na baa la njaa.