Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

udadavuzi

Mabadiliko ya tabianchi yanachangia hali ya ukame katika maeneo mbalimbali duniani.
© WMO/Fouad Abdeladim

UDADAVUZI: COP28 ni nini, na kwa nini ni muhimu?

Hali ya joto duniani inaendelea kufikia viwango vya juu na kuvunja rekodi na, mwaka unavyofikia ukingoni, joto la kidiplomasia linaongezeka huku macho yote yakielekezwa Dubai, Falme za Kiarabu, ambako viongozi wa dunia wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba, ili kutathmini njia za kusonga mbele katika vita vya dunia dhidi ya mabadiliko tabianchi.

Mashambulizi ya makombora dhidi ya Gaza yanaendelea. (Maktaba)
© UNICEF/Eyad El Baba

UDADAVUZI GAZA: Nini kitafuata baada ya mkwamo Barazani?

Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! Marekani ikitumia kura turufu. Sasa nini kinafuatia? Rasimu mpya au kikao cha dharura cha Baraza Kuu? 

Sauti
3'51"
Umoja wa Mataifa unaendelea kusaidia wapalestina walionasa kwenye mapigano  yanayoendelea Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati
© UNRWA

UDADAVUZI: Jinsi UN inavyofanya kazi "nyuma ya pazia" wakati wa migogoro

Safari inayosubiriwa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres kwenda Misri kukutana na Rais Abdel Fattah Al Sisi ni juhudi za hivi karibuni zaidi miongoni mwa juhudi kubwa za Umoja wa Mataifa za kila wakati za kushughulikia mzozo unaoendelea kati ya Gaza na Israel, athari zake zinazoendelea katika nchi jirani za Lebanon na Syria, na vikwazo vya kupeleka msaada wa kuokoa maisha katika eneo la Palestina lililozingirwa.

 

Lori likiwa limejaa chupa za maji ya kunywa  likielekea Al Arish mji ulio kilometa 32 kusini mwa mpaka wa Gaza
© UNICEF/Mohamed Ragaa

Udadavuzi: Kuna nini ndani ya msafara wa misaada kwenye kivuko cha Gaza

Chini ya kilomita moja kutoka Gaza, vibao vya kuengeshean chakula, mafuta, maji, na dawa ni miongoni mwa mamia ya tani za misaada ya kuokoa maisha iliyopakiwa kwenye msafara mrefu wa malori yakiwa yamesimama kwenye upande wa Misri wa kivuko cha mpakani ch a Rafah, huku madereva wakisubiri ruksa ya Israel ili waweze kufikia Wapalestina milioni 2.3 waliozingirwa na walionaswa katika mzozo wa vita vinavyoendelea.