COP30: Rais wa Baraza Kuu la UN atembelea uzalishaji wa kakao unaolinda misitu
Kwenye Ilha do Combu, pembezoni mwa Belém, Annalena Baerbock Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekutana na Dona Nena, mfanyabiashara aliyebadilisha maarifa ya jadi kuwa chanzo cha mapato katika eneo la kando ya mto, wamezungumza kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi, ambazo zinakausha miti, matunda na kuathiri biashara.