Nchi zinazoendelea zihusishwe katika maamuzi ya mageuzi ya mifumo ya fedha:Uganda
Nchi zinazoendelea zihusishwe katika maamuzi ya mageuzi ya mifumo ya fedha:Uganda
Uganda imekuwa mstari wa mbele katika ukarimu wa kupokea na kukumbatia wimbi kubwa la wakimbizi kutoka ndani ya kanda na hata imeorodheshwa kama moja ya nchi inayopokea na kuhifadhi wimbi kubwa la wakimbizi duniani. Hivyo ndivyo alivyoanza hotuba yake makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo alipohutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jioni ya leo jijini New York Marekani.
Hata hivyo Bi. Alupo ameushukuru Umoja wa Mataifa, nchi wanachama wa Umoja huo na wadau wa maendeleo kwa uungaaji mkono wao na msaada wanaoutoa kwa serikali ya Uganda lakini pia kwa wakimbizi.
Kutokana na changamoto zinazoletwa na mzigo wa wakimbizi mwakamu huyo wa Rais wa Uganda amesema wanafanyakazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa na washirika wengine ili kushughulikia mizizi ya watu kutawanywa.
Changamoto za kifedha
Kuhusu masuala ya maendeleo kwa mujibu wake nchi za Dunia ya tatu zinaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya masuala ya kifedha hali ambayo inaathiri uwezo wao wa kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.
Amesisitiza kwamba “ Tunaamini kwamba hitaji la dharura la kufanya mageuzi ya usanifu wa fedha wa kimataifa ni la msingi na muhimu katika kushughulikia changamoto hizi. Marekebisho haya lazima yawe makubwa ili kuhakikisha kuwa nchi zinazoendelea zinawakilishwa vyema na kushiriki ipasavyo na kwa ufanisi katika kufanya maamuzi ya taasisi hizi za fedha za kimataifa.”
Kwa hotuba kamili bofya hapa