Ukanda wa Gaza: Kampeni ya chanjo kwa watoto yazinduliwa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF, afya duniani WHO, linalohudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA na wizara ya afya ya Palestina wamezindua kampeni maalum ya chanjo, lishe na ufuatiliaji wa ukuaji wa watoto katika Ukanda wa Gaza, lengo likiwa ni kuwafikia watoto 44,000 waliokosa huduma muhimu za afya kutokana na vita vilivyodumu kwa miaka miwili.