Siku za UN

22 Februari 2021

U hali gani siku ya leo Jumatatu Februari 22 mwaka 2021 na mwenyeji wako Flora Nducha anakueletea mada kwa kina akimulika lugha ya mama, kwa kuzingatia kuwa tarehe 21 mwezi Februari ni siku ya lugha ya mama duniani.

Sauti -
11'7"

Tukiadhimisha siku ya lugha ya mama tuhakikishe ujumuishi wake shuleni na katika jamii:UNESCO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya lugha ya mama, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO limehimiza watu kila mahali kukumbatia utofauti uliopo duniani kwa kuunga mkono lugha mbalimbali mashuleni na katika maisha ya kila siku.

Haki ya kijamii inastahili pia katika uchumi wa kidijitali:UN 

Katika kuadhimisha siku ya haki ya kijamii duniani leo Februari 20, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa kuziba pengo la kidijitali lililozidishwa na janga la corona au COVID-19 na kuratibu kanuni za kazi katika majukwaa ya kidijitali. 

Radio inakwenda na wakati kukidhi mahitaji ya jamii- UNESCO

Leo ni siku ya redio duniani, siku ambayo huadhimishwa kila tarehe 13 ya mwezi Februari kutoa fursa ya kuangazia mabadiliko, ubunifu na uunganishaji wa chombo hicho ambacho kimetimiza miaka 110.
 

Kuengua wanawake kwenye sayansi ni sawa na kukwamisha Ajenda 2030- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kusongesha usawa wa jiinsia katika nyanja ya sayansi na teknolojia ni muhimu kwa ajili ya kujenga mustakabali bora zaidi.
 

Hata waliposema uhandisi ni kwa wanaume, sikukata tamaa- Francine

Udadisi wangu katika magari ulinichochea kuwa mhandisi wa magari- Francine

Sauti -
2'38"

11 Februari 2021

Hii leo Jaridani Grace Kaneiya kutoka Nairobi Kenya anaanza Habari za UN akimmulika msichana kutoka Rwanda ambaye ni mhandisi wa magari kwenye kampuni ya magari ya Hyundai kwenye mji mkuu Kigali, ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi.

Sauti -
13'38"

Mikunde kwa lishe na kipato!

Ikiwa leo ni siku ya mikunde duniani, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa

Sauti -
1'48"

10 Februari 2021

Jaridani hii leo Flora Nducha anaanza na taarifa ya changamoto kwa watengeneza chanjo dhidi ya COVID-19 duniani wakati huu ambapo chanjo za sasa zimeonekana kuwa dhaifu kwa mnyumbuliko mpya wa

Sauti -
12'4"

Mikunde ni suluhu ya njaa na kulinda mazingira:FAO 

Ikiwa leo ni siku ya mikunde duniani, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuna kila sababu ya kuipenda mikunde sio tu kwa kuwa suluhu ya njaa bali pia uwezo wake wa kulinda na kuhifadhi mazingira.