Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 SEPTEMBA 2023

19 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Leo ni siku ya pili na ya mwisho wa mkutano kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs lakini leo pia ndio pazia la mjadala Mkuu wa 78, UNGA78 limefunguliwa na pamoja na na hotuba za viongozi pia kutakuwa na mikutano itakayo jadili hali za ulinzi na usalama katika mataifa mbalimbali na hapo kesho kutakuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Sudan. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na nashinani ikimulika hotuba za viongozi katika Baraza Kuu na kazi za vijana katika utekelezaji wa DGs.  

  1. Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, limefungua pazia leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuja na azimio la kisiasa la kuhakikissha wanayanusuru malengo hayo ambayo mengi yanakwenda mrama kwani ni asilimia 15 pekee kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndio yametimizwa huku ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufikia mwaka 2030 ukomo wa utimizaji wa malengo hayo.
  2. Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030.   
  3. Makala nampisha Thelma Mwadzaya na makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs.
  4. Kama kawaida Rais wa kwanza kuhutubia ni wa Brazil akifuatiwa na Marekani. Pia Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine yuko hapa akiwa miongoni mwa wanaoutubia leo. Aidha ratiba inaonesha kwa leo siku ya ufunguzi marais kutoka bara la Afrika watakaohutubia ni Rais wa Afrika Kusini, Msumbiji, Nigeria, Senegal. Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanaonekana kwenye ratiba ya kesho.
  5. Mashinani tunasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York kusikia jinsi ambavyo vijana wanavyochangia katika mchakato wa kusongesha ajenda ya malengo ya malengo endelevu. 

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'34"