Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

24 APRILI 2024

Karibu kusikiliza jarida hii leo linaangazia masuala mbalimbali ikiwemo ripotoi ya mgogoro wa chakula duniani, kuanza kwa wiki ya chanjo na utoaji chanjo kwa watoto mashinani. 

Sauti
10'

23 APRILI 2024

Hii leo jaridani utasikia kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP.

Pia utasikia muhtasari wa habari kuhusu wasaka hifadhi huko nchini Uingereza kuhamishiwa Rwanda, Makaburi ya halaiki huko Gaza na kuongezeka kwa mlipuko wa ugonjwa wakipindi pindu duniani.

Kwa upande wa mashinani hii leo utasikia kuhusu harakati za mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali katika kuhakikisha usalama wa mipaka.

Sauti
10'49"

19 APRILI 2024

Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kufanikisha kuhamia katika nishati jadidifu - Francesco La Camera.

Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza: Joram Nkumbi na Vivian Joseph.

Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT – Tanzania.

Mashinani ni nchini Kenya kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ukulima endelevu na mikopo ya fedha katika mzunguko wa kijamii (Merry-go) inavyowasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Audio Duration
14'40"