Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kashmir ni ufunguo wa Amani kati ya Pakistan na India: Waziri Mkuu wa Pakistan

Waziri Mkuu wa Pakistan Anwaar-ul-Haq Kakar akuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Mkutano wake wa 78 jijini New York Marekani.
UN Photo/Cia Pak
Waziri Mkuu wa Pakistan Anwaar-ul-Haq Kakar akuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Mkutano wake wa 78 jijini New York Marekani.

Kashmir ni ufunguo wa Amani kati ya Pakistan na India: Waziri Mkuu wa Pakistan

Amani na Usalama

Waziri Mkuu wa Pakistan Anwaar-ul-Haq Kakar amesema dunia inashuhudia mizozo ikiendelea nchini Ukraine na maeneo mengine 50 duniani kote na kwamba haiwezi tena kuhimili vita nyingine baridi hususan za kikanda kwani kuna changamoto lukuki zinazowakabili wanadamu ambazo zinahitaji ushirikiano ili kuzitatua. 

Akuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Mkutano wake wa 78 jijini New York Marekani waziri Mkuu Kakar amesema kutokana na hitaji la kuwa na maendeleo na kusaidia wananchi wote “Pakistan inatamani kuwa na uhusiano wa amani na wenye tija na majirani zetu wote, pamoja na India.”

Akizungumzia mgogoro unaoendelea huko Jammu na Kashmiri Waziri Mkuu huyo amesema “Kashmir ndio ufunguo wa amani kati ya Pakistan na India.” na kwamba sasa ni muda wa kumaliza mgogoro huo ambao umekuwa ukizungumzwa kwa muda mrefu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Waziri Mkuu huyo ametaja juhudi kadhaa zinazofanywa na nchi hiyo katika kuendeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs nakuhimiza amani itakayosengesha zaidi “Maendeleo yanategemea amani. Pakistani iko katika moja ya kanda ambazo hazina muungano imara wa kiuchumi duniani. Pakistan inaamini kuwa mabara yanakuwa pamoja.” 

Akizungumzia masuala ya ugaidi ameleeza nchi yake inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kupamba na magaidi ndani na nje ya nchi hiyo. 

Islamophobia

Waziri Mkuu huyo wa Pakistan Anwaar-ul-Haq Kakar amezungumzia pia chuki dhidi ya Uislamu na vitendo vya kuchoma moto Qur'ani Tukufu na kupongeza Azimio lililopitishwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa lililopendekezwa na Pakistan kwa niaba ya jumuiya ya ushirikiano wa Kiislamu OIC, na kutangaza Machi 15 kama Siku ya Kimataifa ya Kupambana na chuki dhini ya Uislamu. 

“Mapema mwaka huu, Baraza la Haki za Binadamu lilipitisha azimio la OIC lililowasilishwa na Pakistan, likiyataka Mataifa kuharamisha uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu na chokochoko kama hizo.”

Waziri Mkuu huyo ameahidi kwamba Pakistan na nchi za OIC zitapendekeza hatua zaidi za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mjumbe Maalum, kuundwa kwa Kituo cha takwimu cha chuki dhidi ya Uislamu, usaidizi wa kisheria kwa waathiriwa na mchakato wa uwajibikaji kuadhibu uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu.

Kutazama video yote ya hotuba yake bofya hapa.