Skip to main content

UNGA78

MKUTANO WA 78 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA78

Jukwaa  limeandaliwa kwa ajili ya mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati ulimwengu ukiendelea kukabiliwa na mdororo wa kijamii na kiuchumi kutokana na Covid 19 na athari zinazoendelea za vita nchini Ukraine, mjadala utafanyika kikamlifu ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019, na viongozi wa ulimwengu wakielekea NY kuwasilisha kauli zao katika Ukumbi mashuhuri. 

Hapa, Habari za UN inakupa kiti cha mstari wa mbele katika shughuli zote. Katika simu yako ya mkononi au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapofafanua hatua dhidi ya changamoto kubwa zaidi duniani na kushiriki katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hatua kabambe ya kumaliza janga la tabianchi, na vikao vitatu vya ngazi ya juu visivyo na kifani kuhusu afya: maandalizi dhidi ya majangahuduma ya afya kwa wote; na mapambano ya kimataifa dhidi ya kifua kikuu

Tutembelee kwenye majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

Twitter: twitter.com/HabarizaUN

Youtube: https://www.youtube.com/@UNNewsKiswahili 

Waziri wa mambo ya nje wa India, Subramaniam Jaishankar, akihutubia kikao cha 78 cha mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
UN Photo/Cia Pak

Katika enzi zilizoghubikwa na ubaguzi, mizozo na migawanyiko, diplomasia ndio suluhu pekee ya ufanisi: India

Waziri wa mambo ya nje wa India, Subramaniam Jaishankar, akihutubia kikao cha 78 cha mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo amesema kuwa katika wakati ambapo dunia inapitia misukosuko isiyo na kifani kuanzia mgawanyiko kati ya ulimwengu wa Mashariki na Magharibi unaoongezeka, na mvutano wa kimataifa baina ya Ulimwengu wa Kaskazini na Kusini kuzidi kuongezeka, diplomasia na mazungumzo ndio suluhisho pekee la ufanisi la kukabiliana na changamoto za sasa.

UN News

Tuna imani Tanzania tutafikia lengo la huduma za afya kwa yote 2030: Waziri Ummy

Tanzania taifa lililo Afrika Mashariki limesema limejipanga vyema katika kutekeleza azimio la kuchukua hatua kuhusu huduma za afya kwa wote lililoidhinishwa kwa kauli moja mwishoni mwa juma na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alikuwa miongoni mwa waliohudhuria na ameketi chini na Flora Nducha wa Idhaa hii na kumfafanulia mikakati yao ya kutekeleza azimio hilo.

Sauti
5'52"
UN News

Msukumo dhidi ya TB ufanane na ule wa COVID-19- Waziri Wafula

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya Kifua Kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo dunia itashikamana na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19. Waziri Wafula alizungumza na Flora Nducha wa Idhaa  hii ya Umoja wa Mataifa.

Sauti
8'40"
Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Isdor Mpango akihutubia katika mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. (21 Sept 2023).
UN Photo/Cia Pak

‘Jicho kwa jicho, huacha kila mtu kipofu’ – Makamu wa Rais wa Tanzania katika UNGA 78

Msemo wa wahenga, “Jicho kwa jicho huacha kila mtu kipofu” umepata nafasi katika ukumbi maarufu wa kihistoria wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa nchini Marekani pale ambapo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango ameutumia msemo huo akisisitiza amani ulimwenguni alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa saa za jioni jijini New York.