Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania tumepiga hatua kubwa kupambana na kifua kikuu: Waziri Ummy Mwalimu

Tanzania tumepiga hatua kubwa kupambana na kifua kikuu: Waziri Ummy Mwalimu

Pakua

Kifua kikuu au TB ni moja ya changamoto kubwa za kiafya duniani na janga ni kubwa zaidi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO duniani kote, TB ni sababu ya 13 inayoongoza kwa vifo na ya pili muuaji wa magonjwa ya kuambukiza baada ya COVID-19 ikiwa juu ya VVU na Ukimwi. Shirika hilo linakadiria kwamba mwaka 2021, takriban watu milioni 10.6 waliugua kifua kikuu kote duniani wakiwemo wanaume milioni sita, wanawake milioni 3.4 na watoto milioni 1.2. Na shirika hilo loimesisitiza kuwa TB iko katika nchi zote na inaathiri makundi ya umri wote ndio maana wakati wa mkutano mkuu wa Baraza Kuu mwezi septemba TB ilikuwa moja wa mada zilizojadiliwa kandoni na mjadala wa Baraza Kuu ukizitaka nchi kuchukua hatua kuutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. Tanzania ilishiriki mkutano huo na waziri wake wa afya ummy Mwalimu alimweleza Flora Nducha wa idhaa hii ya Kiswahili hatua wanazochukua katika vita dhidi ya TB.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Flora Nducha
Sauti
3'39"
Photo Credit
UN News