Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

HLPF: Je, Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania imewasilisha nini?

Mhandisi Cyprian John Luhemeja, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania.
UN News/Anold Kayanda
Mhandisi Cyprian John Luhemeja, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania.

HLPF: Je, Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania imewasilisha nini?

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ikiwa leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs limeingia siku yake ya nne na linategemewa kuendelea hadi tarehe 17 ya mwezi huu wa Julai, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wametuma wawakilishi kutoka katika serikali zao ili kushiriki mkutano huu muhimu. 

Je, Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania imewasilisha nini kwenye jukwaa hili? Katika mahojiano na Anold Kayanda wa Idhaa hii, Katibu Mkuu Mhandisi Cyprian John Luhemeja anaeleza.

Mahojiano haya yamefanyika katika Makao makuu ya Umoja wa Mataifa Julai 10 2024 mara tu baada ya Bwana Luhemeja kuwasilisha kwa wajumbe taarifa kutoka Tanzania.