Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UNIS/Stella Vuzo

UNEA6 ni mwongozo wa kushirikisha pande zote katika kulinda mazingira: Irene Mwoga

Mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 leo umefungua pazia katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Nairobi, nchini Kenya.  Mkutano huo utakaodumu kwa siku tano unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 6000 ikiwa ni pamoja na viongozi wa Mazingira duniani, asasi za kiraia, wataalamu wa Mazingira, maofisa waserikali za mitaa, wakulima, vyama vinavyowakilisha wafanyakazi, jamii zilizoachwa nyuma pamoja na maofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.

Sauti
2'23"
UN News

Kiswahili kuanza kutumika EAC rasmi mwaka 2024

Lengo namba 17 la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs linataka uwepo wa Ushirikiano katika kufanikisha malengo. Ushirikiano huo unaweza kuwa baina ya nchi na nchi, wananchi na ushirikiano wa kikanda. Mwezi Desemba mwaka jana 2023 nilifunga safari hadi jijini Arusha nchini Tanzania na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki kutaka kufahamu namna wanavyoshirikiana na Umoja wa Mataifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ulinzi na usalama pamoja na kukuza lugha ya Kiswahili. Karibu usikilize mazungumzo yetu. 

Sauti
7'40"
Pan American Health Organization

Saratani ya shingo ya kizazi inatibika ikigundulika mapema – WHO

Mwezi huu wa januari umetangazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO kuwa ni mwezi wa kujenga ufahamu kuhusu ugonjwa wa Saratani ya shingo ya Kizazi, nami nimemualika mwenzangu Leah Mushi hapa studio ambaye amefuatilia kwa kina suala hilo kupitia wavuti wa WHO.

Swali: Leah kwanza tueleze lipi hasa WHO wanalotaka wadau wafanye?

Jibu: WHO inahamasisha mambo makuu 3 mosi, kutoa taarifa kuwa kuna ugonjwa huo, pili kuhimiza uchunguzi na tatu kuhamasisha chanjo. 

Sauti
1'59"
UN News/Assumpta Massoi

Siri ya kuwa sehemu ya tuzo hii ni ushirikiano wetu - Fr. Benedict Ayodi

Hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika hafla la kupatia tuzo washindi wa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, tuzo inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja au kundi kwa kuzingatia mchango wao kwenye kusongesha haki za binadamu. Miongoni mwa washindi wa watano ni Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika ya kijamii, watu wa asili, harakati za kijamii na jamii za mashinani. Shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Wafransiskani wakapuchini ni sehemu ya ushirikiano huo.

Sauti
7'46"
UN News/George Musubao

MONUSCO na ufanikishaji wa uchaguzi mkuu wa 2023 DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (MONUSCO) unashiriki katika maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ambapo tayari umeshasaidia usafirishaji wa nyaraka za uchaguzi, halikadhalika mafunzo kwa polisi wa kitaifa ili uchaguzi huo uwe huru na ufanyike kwa amani.

Sauti
4'53"
UN News

Tuna imani Tanzania tutafikia lengo la huduma za afya kwa wote 2030: Waziri Ummy

Tanzania taifa lililo Afrika Mashariki limesema limejipanga vyema katika kutekeleza azimio la kuchukua hatua kuhusu huduma za afya kwa wote lililoidhinishwa kwa kauli moja mwishoni mwa juma na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alikuwa miongoni mwa waliohudhuria na ameketi chini na Flora Nducha wa Idhaa hii na kumfafanulia mikakati yao ya kutekeleza azimio hilo.

Sauti
5'52"
UN News

Msukumo dhidi ya TB ufanane na ule wa COVID-19- Waziri Wafula

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya Kifua Kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo dunia itashikamana na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19. Waziri Wafula alizungumza na Flora Nducha wa Idhaa  hii ya Umoja wa Mataifa.

Sauti
8'40"
UN News

Tunaelimisha wanafunzi na vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi - Madina Jubilate Kimaro

Wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Madina Jubilate Kimaro, Balozi wa Mazingira wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Tanzania.

Sauti
6'24"
UN News

Mradi wa "Football for the Goals" kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu Rwanda - UN Rwanda

Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia chepuo mbinu mbali mbali halali za kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, na miongoni mwa mbinu hizo ni mpira wa miguu, soka, wengine wakisema kabumbu au kandanda! Sasa wenyewe wabobezi au manguli wa soka wameitikia wito na Umoja wa Mataifa hususan nchini Rwanda ukaitikia Naam!!! Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ameketi na Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa UN, Rwanda Josephine Marealle-Ulimwengu na anafafanua kitendawili hicho.

Sauti
6'43"