Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio la kisiasa la kuchukua hatua lapitishwa kuhakikisha huduma za afya kwa wote: UN

Mama kijana akimtunza mtoto wake katika chumba cha wagonjwa mahututi wachanga huko Mbeya, Tanzania.
© UNICEF/Reinier van Oorsouw
Mama kijana akimtunza mtoto wake katika chumba cha wagonjwa mahututi wachanga huko Mbeya, Tanzania.

Azimio la kisiasa la kuchukua hatua lapitishwa kuhakikisha huduma za afya kwa wote: UN

Afya

Viongozi wa dunia leo ameahidi kuongeza mara mbili juhudi zai katika kuelekea huduma za afya kwa wote UHC, ifikapo mwaka 2030.

Wakikutana katika mkutano wa ngazi ya juu kandoni mwa mjadala wa Baraza Kuu UNGA78 wamepitisha azimio jipya la kisiasa liliafikiwa awali kuhusu Huduma za Afaya kwa wote, likipanua wigo wa matamanio kwa ajili ya afya na ustawi wa kila mtu baada ya Ulimwengu wa janga la coronavirus">COVID-19.

Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa ambalo ndio mwaandaji wa mkutano huo azimio hilo limesifiwa kama kichocheo muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kubwa na za ujasiri na kuhamasisha ahadi muhimu za kisiasa na uwekezaji wa kifedha ili kufikia lengo la UHC la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs ifikapo 2030.

Lengo kuu la UHC

Lengo la UHC ni hupima uwezo wa nchi kuhakikisha kwamba kila mtu anapata huduma ya afya anayohitaji, wakati na mahali anapohitaji, bila kukabiliwa na  matatizo ya kifedha. 

Pia linashughulikia mwendelezo kamili wa huduma muhimu kuanzia uhamasishaji wa afya hadi kinga, ulinzi, matibabu, urekebishaji na huduma za uponyaji. Shirika hilo limesema inashangaza kwamba maendeleo ya kimataifa kuelekea UHC yamekuwa yakidumaa kwa kiasi kikubwa tangu 2015, kabla ya kukwama zaidi katika 2019.

Udharura wa azimio hilo unadhihirika katika takwimu za kushangaza. WHO inasema angalau watu bilioni 4.5 zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani hawakuhudumiwa kikamilifu na huduma muhimu za afya mwaka wa 2021. 

Watu bilioni mbili walipata matatizo ya kifedha, huku zaidi ya watu bilioni 1.3 wakisukumwa au kuingizwa kwenye umaskini wakijaribu tu kupata huduma za msingi za afya ukweli dhahiri wa kuongezeka kwa pengo la usawa wa afya.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema “Hatimaye, huduma ya afya kwa wote ni chaguo, ni chaguo la kisiasa. Azimio hilo la kisiasa zilizoidhinishwa leo nan chi ni ishara tosha kwamba zinafanya chaguo hilo. Lakini uchaguzi haufanyiki tu kwenye karatasi. Unafanywa katika maamuzi ya bajeti na maamuzi ya sera. Zaidi ya yote, unafanywa kwa kuwekeza katika huduma za afya ya msingi, ambayo ndiyo njia inayojumuisha zaidi, ya usawa, na yenye ufanisi kwa huduma za afya kwa wote."

Kigezo cha kubadili mwelekeo

Katika azimio hilo la Kisiasa, wakuu wa nchi na viongozi wa dunia wamejitolea kuchukua hatua muhimu za kitaifa, kufanya uwekezaji muhimu, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na mshikamano wa kimataifa katika ngazi ya juu ya kisiasa ili kuharakisha maendeleo kuelekea UHC ifikapo 2030, kwa kutumia mbinu ya afya ya msingi PHC.

Ili huduma ya afya iwe ya ulimwengu wote, WHO imesema inahitajika kuhama kutoka kwenye mifumo ya afya iliyojikita katika mazingira ya magonjwa na kuhamia kwenye mifumo iliyojikita kwa ajili ya watu. 

PHC, mbinu ya kuimarisha mifumo ya afya inayozingatia mahitaji ya watu, ni mojawapo ya maeneo yenye ufanisi zaidi kwa uwekezaji ili kuharakisha maendeleo kuelekea UHC limesisitiza shirika hilo.

Nchi ambazo zimechukua mtazamo wa PHC zina uwezo bora wa kujenga kwa haraka mifumo imara na thabiti ya afya ili kufikia walio hatarini zaidi na kupata faida kubwa zaidi kwenye uwekezaji wa afya. 

Muhimu zaidi, wanahakikisha kwamba watu wengi zaidi wanahudumiwa na huduma muhimu za afya na wanawezeshwa kushiriki katika kufanya maamuzi yanayoathiri afya na ustawi wao.

Dola bilioni 200-328 zaidi zitahitajika kila mwaka 

Inakadiriwa kuwa uwekezaji wa ziada wa kati ya dola bilioni 200-328 kwa mwaka unahitajika ili kuongeza mbinu ya PHC katika nchi za kipato cha chini na cha kati takriban asilimia 3.3 ya pato la taifa. 

Hii inaweza kusaidia mifumo ya afya kutoa hadi asilimia 90 ya huduma muhimu za afya, kuokoa maisha ya watu milioni 60 na kuongeza wastani wa maisha kwa miaka 3.7 ifikapo 2030.

WHO, kupitia mtandao wake wa zaidi ya ofisi 150 za nchi na ofisi sita za kikanda, hutoa usaidizi wa kiufundi ili kuharakisha uelekezaji upya wa mifumo ya afya kupitia mbinu zinazolenga PHC, na kuhakikisha mwongozo thabiti kufuatilia maendeleo ya uwajibikaji na athari.

Heko nchi wanachama kupitisha azimio hili

WHO inazipongeza nchi wanachama kwa kuidhinisha azimio la pili la kisiasa la mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu UHC, ambalo lilitayarishwa kupitia mchakato mpana wa mashauriano. 

WHO imejitolea kikamilifu kufanya kazi na nchi wanachama na washirika ili kuimarisha hatua za sera kwa ajili ya UHC na kupanua wigo wa huduma, kuhakikisha ulinzi wa kifedha na kuunda usanifu wa kifedha ili kuwekeza zaidi na kwa ubora zaidi katika afya.

Mara baada ya kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, azimio hilo la kisiasa litafuatiliwa mara kwa mara kwa ajili ya utekelezaji ili kutambua mapungufu na ufumbuzi wa kuharakisha maendeleo, na kujadiliwa katika Mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa wa ngazi ya juu mwaka 2027.