Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA77

MKUTANO WA 77 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA77

Mambo sasa yameiva kwa ajili ya Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati dunia inaanza taratibu kujikwamua kutoka katika janga baya kabisa la coronavirus">COVID-19, mjadala wa ngazi ya juu wa mkutano wa 77 kwa kiasi kikubwa utafanyika kwa viongozi kuweko kwenye ukumbi mashuhuri wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, tofauti ya miaka miwili iliyopita ambapo viongozi wengine walikuweko ukumbini na wengine walitoa hotuba zao kwa njia ya video. 
 
Katika ukurasa huu, Habari za UN itakupatia kiti cha mbele kabisa kutoka kwenye kumbi zote. Kupitia simu yako ya kiganjani au rununu bila kusahau kompyuta yako au kishkwambi, utafuatilia hotuba za wakuu wa nchi na serikali wakati wakitoa ainisho au majawabu ya changamoto zinazokabili Dunia hivi sasa, sambamba na wanavyoshiriki katika mkutano wa ngazi ya juu wa Marekebisho ya Mfumo wa Elimu, kushughulikia janga la chakula duniani, maadhimisho ya miaka 30 ya Azimio la UN kuhusu haki za watu wa makabila madogo halikadhalika mzozo wa Ukraine.

Rambaza kwenye majukwaa yetu ya mitando ya kijamii

Twitter: Habari za UN
Youtube: Habari za UN

Emmanuel Cosmas Msoka, Mchechemuzi wa Vijana wa UNICEF Tanzania kuhusu usafi wa maji, usafi wa mazingira (WASH) na ubunifu.
UN/Anold Kayanda

Maneno ni bei nafuu sana lakini vitendo ni bei ghali, tushirikishe vijana kwa vitendo:Msoka  

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu leo unakunja jamvi kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani. Mkutano huo wa siku tatu umeitishwa ili kukabiliana na changamoto ya kimataifa ya elimu hasa kwa kuzingatia suala la usawa na ujumuishwaji, ubora wa elimu na umuhimu.  

Sauti
2'23"
Kikundi cha ushirika cha wanawake cha kuchakata dagaa nchini Senegal
UN Women/BrunoDemeocq

Afrika haishikiki, haizuiliki, asema Katibu Mkuu UN akizindua GABI

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika uzinduzi wa mpango wa kimataifa wa kuimarisha biashara barani Afrika, Global African Business Initiative, GABI,  wenye lengo la kuchagiza fursa za kibiashara na kukwamua bara hilo kiuchumi, bara ambalo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni sehemu muhimu ya biashara duniani na eneo kubwa la uwekezaji.

Wanafunzi wakiwa darasani wilaya ya Kasese nchini Uganda.
© UNICEF/Maria Wamala

Elimu bora ni 'tofali' la jengo bora la amani, utulivu na maendeleo- Katibu Mkuu UN

Mkutano wa kimataifa wa marekebisho ya mfumo wa elimu ukiwa umeingia siku ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa wahisani kuchangia fedha zaidi ili kukwamua sekta ya elimu ambayo sasa inakumbwa na changamoto lukuki hususan katika nchi zinazoendelea.

Watoto wakihudhuria darasa na vishkwambi katika shule ya Radi, katika kijiji cha Safi, Kusini mwa Niger.
© UNICEF Frank Dejongh

Viongozi wastaafu wapendekeza kuanzishwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa Elimu

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya elimu ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, zaidi ya viongozi 100 wameandika barua wakitaka mkutano huo utenge rasilimali za kushughulikia janga la elimu duniani na halikadhalika uahidi mikakati ya kijasiri ya kufanikisha kizazi cha kwanza katika historia ambacho kila mtoto anakwenda shule.

Csaba Kőrösi, Rais wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA77
UN /Cia Pak

Mahojiano: Csaba Kőrösi, Rais wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la UN

Rais wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi amesema dunia hivi sasa inakumbwa na machungu na matatizo makubwa kutokana na ukosefu wa imani na kwamba “wakati tunapanga kuhusu kuchungua hatua kusongesha dunia mbele kutoka katika changamoto hizi lukuki, kuanzia mabadiliko ya tabianchi hadi vita ya Ukraine na uhaba wa chakula,” atatumia mamlaka yake kuongoza chombo hicho cha UN ili kusaidia kurejesha imani miongoni mwa mataifa na kuimarisha imani kwa mfumo wa kimataifa.



 

© UNICEF/Juan Haro

Walimu wasio na sifa ni moja ya sababu za janga la elimu duniani- UNICEF

Mkutano wa Ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu duniani ukianza leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa taarifa inayoeleza idadi ya Watoto wasiojua kusoma imeongezeka ulimwenguni ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Assumpta Massoi

Sauti
2'31"
Taswira wa darasa la mfano linalolenga kuonesha Mgogoro wa kujifunza duniani. Darasa hili lililoandaliwa na UNICEF liko makao makuu ya UN jijini New York, Marekani.
© UNICEF/Chris Farber

Mtoto 1 kati ya 3 duniani kote ndiye awezaye kusoma na kuelewa hadithi fupi na hali si shwari - UNICEF

Mkutano wa Ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu duniani ukianza leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa taarifa inayoeleza idadi ya Watoto wasiojua kusoma imeongezeka ulimwenguni ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita. 

Sauti
2'31"
Mama na mwanae wakiondoka kituo cha treni cha Lvivi nchini Ukraine.
© UNICEF/Giovanni Diffidenti

"Katika zama za mitikisiko, dhima ya UN ni muhimu kuliko wakati wowote," Katibu Mkuu UN

Kipindi cha mwaka mmoja uliopita kimekuwa cha majanga yaliyoingiliana na makubwa na ambayo yameendelea kuongezeka kwa ukumbwa na makali yake, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, akitaja janga la COVID-19, vita nchini Ukraine, kuongezeka kwa janga la tabianchi.  Amesema majanga hayo yamevuka mipaka na yamefanya dhima ya Umoja wa Mataifa kuwa muhimu zaidi kuliko wakati wowote.