Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA77

MKUTANO WA 77 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA77

Mambo sasa yameiva kwa ajili ya Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati dunia inaanza taratibu kujikwamua kutoka katika janga baya kabisa la COVID-19, mjadala wa ngazi ya juu wa mkutano wa 77 kwa kiasi kikubwa utafanyika kwa viongozi kuweko kwenye ukumbi mashuhuri wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, tofauti ya miaka miwili iliyopita ambapo viongozi wengine walikuweko ukumbini na wengine walitoa hotuba zao kwa njia ya video. 
 
Katika ukurasa huu, Habari za UN itakupatia kiti cha mbele kabisa kutoka kwenye kumbi zote. Kupitia simu yako ya kiganjani au rununu bila kusahau kompyuta yako au kishkwambi, utafuatilia hotuba za wakuu wa nchi na serikali wakati wakitoa ainisho au majawabu ya changamoto zinazokabili Dunia hivi sasa, sambamba na wanavyoshiriki katika mkutano wa ngazi ya juu wa Marekebisho ya Mfumo wa Elimu, kushughulikia janga la chakula duniani, maadhimisho ya miaka 30 ya Azimio la UN kuhusu haki za watu wa makabila madogo halikadhalika mzozo wa Ukraine.

Rambaza kwenye majukwaa yetu ya mitando ya kijamii

Twitter: Habari za UN
Youtube: Habari za UN

 Csaba Kőrösi, Rais Mteuel wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza Kuu baada ya kuchaguliwa.
UN/ Eskinder Debebe

UNGA77 Mambo 5 muhimu ya kuyafahamu 

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufunguliwa kwa kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jumuiya ya wanadiplomasia ya Umoja wa Mataifa pamoja na wakazi wa jiji la New York wanajiandaa kuwasili kila mwaka kwa Wakuu wa nchi na serikali kutoka sehemu mbalimbali duniani. , baada ya miaka miwili ya usumbufu uliosababishwa na janga la COVID-19.