Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA77

MKUTANO WA 77 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA77

Mambo sasa yameiva kwa ajili ya Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati dunia inaanza taratibu kujikwamua kutoka katika janga baya kabisa la coronavirus">COVID-19, mjadala wa ngazi ya juu wa mkutano wa 77 kwa kiasi kikubwa utafanyika kwa viongozi kuweko kwenye ukumbi mashuhuri wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, tofauti ya miaka miwili iliyopita ambapo viongozi wengine walikuweko ukumbini na wengine walitoa hotuba zao kwa njia ya video. 
 
Katika ukurasa huu, Habari za UN itakupatia kiti cha mbele kabisa kutoka kwenye kumbi zote. Kupitia simu yako ya kiganjani au rununu bila kusahau kompyuta yako au kishkwambi, utafuatilia hotuba za wakuu wa nchi na serikali wakati wakitoa ainisho au majawabu ya changamoto zinazokabili Dunia hivi sasa, sambamba na wanavyoshiriki katika mkutano wa ngazi ya juu wa Marekebisho ya Mfumo wa Elimu, kushughulikia janga la chakula duniani, maadhimisho ya miaka 30 ya Azimio la UN kuhusu haki za watu wa makabila madogo halikadhalika mzozo wa Ukraine.

Rambaza kwenye majukwaa yetu ya mitando ya kijamii

Twitter: Habari za UN
Youtube: Habari za UN

22 SEPTEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anakuletea mada kwa kina, Habari kwa Ufupi na Neno la Wiki.

Habari kwa Ufupi zinamulika harakati za kutumia chanjo inayoweza kukabili virusi aina ya #EbolaSudan nchini Uganda kwa kuwa chanjo ya sasa haina uwezo huo. Pia nafasi ya nishati jadidifu katika kuongeza ajira duniani, ripoti mpya imethibitisha hilo! Kisha wito wa Rais wa Botswana kwenye mjadala mkuu wa UNGA77 wa kutaka wananchi wake nao waajiriwe Umoja wa Mataifa.

Sauti
12'36"
Gibson Kawago

Kiu ya kutafuta nishati salama nyumbani ilisababisha kubuni matumizi ya betri chakavu kutengeneza nishati

Kijana Gibson Kawago kutoka Tanzania ambaye ni miongoni mwa vijana 17 walioteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa viongozi vijana wa kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs amesema atatumia kipindi cha miaka miwili cha nafasi hiyo kusongesha hatua kwa tabianchi ikiwemo kutumia ugunduzi wake kuchakata betri chakavu za kompyuta kutengeneza betri za kuzalisha umeme katika kulinda na kuhifadhi mazingira.  

Nina furaha sana kuteuliwa na nitakuwa balozi mwema 

Sauti
3'23"
Kufanya kazi kwa saa nyingi kunaongeza hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi
ILO /Marcel Crozet

WHO imetaka serikali duniani ziokoe maisha ya watu milioni 50 wanaougua magonjwa yasiyoambukiza, NCDs

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa ulimwengiuni WHO leo kandoni mwa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York Marekani limezindua ripoti mpya inayowataka viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs ambayo hukatili Maisha ya watu milioni 17 kila mwaka.

Sauti
2'22"

21 SEPTEMBA 2022

Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Kandoni mwa mjadala wa wazi wa Umoja wa Mataifa shirika la afya duniani WHO limewataka viongozi wa dunia kuchukua hatua haraka kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs yanayokatili maisha ya watu milioni 50 kila mwaka

-Kijana Mtanzania Gibson Kawago ni miongoni mwa vijana 17 waliotangazwa leo na Umoja wa Mataifa kuwa viongozi vijana wa kusongesha malengo ya maendeleo endelevu SDG's je amepokeaje uteuzi huo na anapanga kufanya nini?

Sauti
13'15"