Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Csaba Kőrösi wa Hungary atakuwa Rais wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu

 Csaba Kőrösi, Rais Mteuel wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza Kuu baada ya kuchaguliwa.
UN/ Eskinder Debebe
Csaba Kőrösi, Rais Mteuel wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza Kuu baada ya kuchaguliwa.

Csaba Kőrösi wa Hungary atakuwa Rais wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu

Masuala ya UM

Mwanadiplomasia Csaba Kőrösi atakuwa Rais wa mkutano wa 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Ni raia wa wa Hungary ambaye amechaguliwa kwa shangwe Jumanne hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani. 

Uchaguzi umefanyika kwa shangwe Jumanne hii; mwanadiplomasia ambaye ana takribani miaka 40 ya kazi, sehemu kubwa ya kipindi hicho akiwa mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa; Utaratibu umeamua kwamba kiongozi wa mkutano ujao wa Baraza Kuu anatoka Ulaya Mashariki. 

Rais wa sasa wa Baraza hilo, Abdulla Shahid, ametoa tangazo la mrithi wake huyo, ambaye kwa mujibu wa sheria, kwas asa alikuwa anazimika kuwa raia wa nchi ya Ulaya Mashariki. Bwana Shahid anayemaliza muda wake anatoka Asia kusini katika nchi ya Maldives.  

Mshikamano 

Csaba Kőrösi ndiye mgombea pekee aliyejitokeza kuchukua nafasi hiyo ya kuongoza kikao kilichofuata, kuanzia Septemba. Kauli mbiu itakuwa "Suluhu kupitia Mshikamano, Uendelevu na Sayansi". 

Kőrösi amesema kuwa jumuiya ya kimataifa lazima itafute suluhu zilizounganishwa kwa mfumo wa Umoja wa Mataifa na changamoto za sasa. Anaiona kama njia pekee ya kutoka katika "hali ngumu" ya kuendelea na mageuzi, na mabadiliko ya shirika na kuimarisha ushirikiano. 

Kwa rais huyu mteule, vita ya Ukraine inaongeza mwelekeo wa changamoto za wakati huu. Ameingeza kuwa mfululizo wa mashauriano na nchi wanachama umesaidia kuunda dira na kuchaguliwa kwake kunathibitisha hatari hizo za kijiografia za maendeleo ya ulimwengu zisizo endelevu zimeanza kuunganishwa na kuimarisha kila mmoja. 

Amesisitiza kuwa vita ya Ukraine na mizozo mingine hinaleta dhoruba kamili na ukosefu wa utulivu kwa miaka ijayo. 

Akiwa na takriban miaka 40 katika diplomasia, ambayo mingi yake akihudumu kama balozi katika Umoja wa Mataifa, Kőrösi alikuwa Mwenyekiti mwenza wa mchakato ulioanzisha Ajenda yam waka 2030 na kufafanua Malengo ya Maendeleo Endelevu. 

Kabla ya kuchaguliwa leo Jumanne Juni, 07, 2022, alikuwa Naibu Katibu wa mambo ya nje nchini Hungary anayehusika na sera za usalama, diplomasia na haki za binadamu. 

Manaibu Rais 

Makamu wa Rais wapya wa kikao kilichofuata ni: Australia, Benin, Burundi, Chile, El Salvador, Israel, Jamaica, Kenya, Malaysia, Mauritania, Nepal, Niger, Tajikistan, Turkmenistan, Vietnam na Zimbabwe.