UNGA77 Mambo 5 muhimu ya kuyafahamu 

10 Septemba 2022

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufunguliwa kwa kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jumuiya ya wanadiplomasia ya Umoja wa Mataifa pamoja na wakazi wa jiji la New York wanajiandaa kuwasili kila mwaka kwa Wakuu wa nchi na serikali kutoka sehemu mbalimbali duniani. , baada ya miaka miwili ya usumbufu uliosababishwa na janga la COVID-19.  

Taarifa nyingi bado zinafanyiwa kazi, lakini hapa kuna mambo matano ya kuyatilia maanani kati ya 12 na 27 Septemba. 

 Csaba Kőrösi, Rais Mteuel wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza Kuu baada ya kuchaguliwa.
UN/ Eskinder Debebe
Csaba Kőrösi, Rais Mteuel wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza Kuu baada ya kuchaguliwa.

 

1. Rais wa Hungary anachukua gavel 

Kikao kipya cha Baraza Kuu kinamaanisha Rais mpya wa Baraza Kuu au PGA kwa kifupisho cha Umoja wa Mataifa .  

Rais wa sasa Abdulla Shahid kutoka Maldives, ataachia ngazi na Csaba Kőrösi wa Hungari atavaa joho hilo kwa muda wa miezi kumi na miwili ijayo. 

Makabidhiano hayo rasmi yatafanyika Jumatatu ya tarehe 12 Septemba ambapo mheshimiwa Shahid atafunga kikao cha 76 cha Baraza Kuu asubuhi, na kikao cha kwanza cha 77  au UNGA77 kinafanyika Jumanne mchana. 

Bwana Kőrösi’s ameshikilia majukumu kadhaa ndani ya wizara ya mambo ya nje ya nchi yake, wadhifa wake wa hivi karibuni kabisa ukiwa mkurugenzi wa uendelevu wa mazingira katika ofisi ya Rais wa Hungaria.  

Amejihusisha na Umoja wa Mataifa kwa miaka kadhaa, na Urais huu pengine hautahusisha mwelekeo mwingi wa kujifunza. 

 

2. Mkutano wa mageuzi ya Elimu 

Kama kawaida, tahadhari ya kimataifa pamoja na idadi kubwa ya polisi, na malalamiko kuhusu msongamano wa magari kutoka kwa wakazi wa New York yatahusu wiki ya mijadala ya ngazi ya juu, itakayoanza Jumanne tarehe 20 Septemba. 

Hata hivyo, mkutano wa kubadilisha elimu, ambao unafanyika wiki moja kabla katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa  utakuwa Ijumaa  ya tarehe 16, Jumamosi  ya tarehe 17 na Jumatatu ya tarehe 19 Septemba unachukuliwa kuwa tukio kuu na Umoja wa Mataifa. 

Ijumaa ni siku ya uhamasishaji, ambayo itaongozwa na vijana na kuandaliwa, kuleta shaka na shuku za vijana juu ya elimu yao kwa wafanya maamuzi na watunga sera, na itazingatia kuhamasisha umma wa kimataifa, vijana, walimu, mashirika ya kiraia na wengine, kusaidia mageuzi ya elimu duniani kote. 

Siku ya pili inahusu masuluhisho, na imeandaliwa kuwa jukwaa la mipango itakayochangia kuleta mabadiliko katika elimu.  

Siku hii imepangwa katika makundi matano (Mada za kuchukua hatua) ambazo ni shule jumuishi, zinazolingana, salama na zenye afya, kujifunza na ujuzi wa maisha, kazi na maendeleo endelevu, walimu, ualimu na taaluma ya ualimu, kujifunza na mabadiliko ya kidijitali, na ufadhili wa elimu. 

Siku ya tatu, ambayo ni Jumatatu tarehe 19 Septemba, ni siku ya viongozi, ikizingatia ukweli kwamba wakuu wengi wa nchi na serikali watawasili New York wiki hiyo.  

Tarajia taarifa nyingi za kitaifa kutoka kwa viongozi hawa. 

Mabango ya SDGs yakiwa katika makao makuu ya UN, jijini New York, Marekani.
UN News/Abdelmonem Makki
Mabango ya SDGs yakiwa katika makao makuu ya UN, jijini New York, Marekani.

 

Siku hiyo pia itakuwa na mkutano wa uwasilishaji wa azimio la vijana wa na taarifa ya dira ya Katibu Mkuu ya mageuzi ya elimu. 

3. Wakati wa SDG 

Wakati wa SDG wa mwaka huu, ambao utafanyika kati ya saa mbili na nusu na saa nne asubuhi Jumatatu Septemba 19, mara moja kabla ya mkutano wa siku hiyo wa viongozi wa mageuzi ya elimu, itakuwa fursa ya kuzingatia tena malengo ya maendeleo endelevu ya ajenda ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa, ambao ni mpango wa mustakabali bora kwa watu na sayari dunia. 

Akizungumza katika Jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu, jukwaa muhimu la maendeleo la kila mwaka mwezi Julai mwaka huu Amina Mohammed, Naibu Katibu Mkuu, alisema kuwa mabadiliko ya nishati mbadala, mifumo ya chakula na muunganisho wa kidijitali pamoja na uwekezaji katika mtaji wa watu, na kufadhili fursa, kunahitajika ili kugeuza mizozo mingi kuwa fursa. 

Bi. Mohammed aliongeza kuwa wakati wa mwaka huu utakuwa "fursa ya kuzingatia mabadiliko haya ya kina, na juu ya kazi inayohitajika ili kuturudisha kwenye mstari wa utimizaji wa malengo hayo. Pia itakuwa hatua muhimu kuelekea mkutano wa 2023 wa SDG.” 

Kipindi cha mwaka jana kilipata umaarufu mkubwa kwa kushirikisha wanamuziki nyota kutoka Korea BTS, ambao walitanabaisha juu ya athari kubwa zilizosababishwa na janga la COVID-19, na kupinga dhana kwamba wao ni sehemu ya kizazi kilichopotea cha COVID. 

Wanawake wa kabila dogo la Lisu, kutoka mkoa wa Yunnan, Uchina, wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni.
UNDP China
Wanawake wa kabila dogo la Lisu, kutoka mkoa wa Yunnan, Uchina, wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni.

 

4. Haki za walio wachache 

Tarehe 18 Desemba 1992, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilipitisha azimio la haki za watu walio wa jamii ndogo za kitaifa au kikabila, kidini na kilugha (Tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za Wachache kwa ufupi), lililoelezwa na Umoja wa Mataifa kama chombo muhimu cha kushughulikia masuala ya kisiasa na haki za kiraia, kiuchumi, kijamii na kitamaduni za watu walio wa wachache. 

Siku ya Jumatano tarehe 21 Septemba, katika chumba cha Baraza la Udhamini, mkutano wa ngazi ya juu utafanyika, kama sehemu ya ukumbusho wa mwaka mzima wa kumbukumbu ya miaka 30 ya azimio hilo. 

Akizungumza mwezi Juni, Paolo David, mkuu wa kitengo cha haki za binadamu za watu wa asili  na walio wanachache cha Umoja wa Mataifa alisema kwamba, wakati kupitishwa kwa azimio hilo kulileta matumaini miongo mitatu iliyopita, hisia hii ilipotea haraka kutokana na mzozo wa silaha katika Yugoslavia ya zamani.  

Bwana David alibainisha kuwa walio wachache wanaendelea kutumiwa katika mizozo mingi, ikiwa ni pamoja na Ukraine, Ethiopia, Myanmar, Sudan Kusini, Syria na Yemen. 

Leo, walio wachache wanakabiliwa na vikwazo na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.  

Katika nchi nyingi wanakabiliana na vitisho vya kisasa kama vile kauli za chuki mtandaoni na wananyang'anywa haki za uraia. 

Tukio hili linachukuliwa kama fursa ya kutathmini vikwazo na mafanikio, kushirikiana mifano ya utendaji bora, na kuweka vipaumbele kwa siku zijazo. 

Malengo ya Maendeleo Endelevu ni mwongozo wa kufikia mustakabali bora na endelevu kwa wote.
© UNDP
Malengo ya Maendeleo Endelevu ni mwongozo wa kufikia mustakabali bora na endelevu kwa wote.

 

5. Wiki ya malengo muniani 

Mjadala Mkuu utaingiliana na wiki ya malengo ya dunia ambayo, licha ya jina hilo, ni programu ya siku tisa ya matukio ya mtandaoni na ya ana kwa ana yanayofanyika kati ya tarehe 16 na 25 Septemba, inayohusisha zaidi ya washiriki 170 kutoka mashirika ya kiraia, biashara, kitaaluma, na mfumo wa Umoja wa Mataifa, ili kuharakisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs). 

Kuna matukio mengi sana ya kuorodheshwa kikamilifu hapa, lakini yanajumuisha wiki ya hali ya hewa ya mji wa New York, inayoangazia changamoto nyingi zinazohusiana na hali ya hewa, Jukwaa la sekta binafsi la Umoja wa Mataifa, linaloendeshwa na UN Global Compact, ambalo linaleta pamoja wafanyabiashara, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia, kushughulikia migogoro ya kimataifa, na uzinduzi wa mradi wa hatua za mabadiliko ya tabianchi wa 2002 kutoka Take Action Global, unaoleta wadau kutoka zaidi ya nchi 140 pamoja, kwa mfululizo wa mahojiano ya moja kwa moja, kutembelea shule na kujitosa kwenye mitandao ya kijamii. 

Kutakuwa na video nyingi za SDG Media Zone za kutazama wakati wa wiki ya malengo ya ulimwengu, kukiwa na wasemaji wengi wanaovutia, wakiwemo waundaji wa maudhui, washawishi, wanaharakati na washirika wa vyombo vya habari, wakishiriki katika mijadala ya kando ambayo itaangazia hatua na suluhisho katika kuunga mkono maendeleo ya maendfeleo endelevu 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter