Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA77

MKUTANO WA 77 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA77

Mambo sasa yameiva kwa ajili ya Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati dunia inaanza taratibu kujikwamua kutoka katika janga baya kabisa la COVID-19, mjadala wa ngazi ya juu wa mkutano wa 77 kwa kiasi kikubwa utafanyika kwa viongozi kuweko kwenye ukumbi mashuhuri wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, tofauti ya miaka miwili iliyopita ambapo viongozi wengine walikuweko ukumbini na wengine walitoa hotuba zao kwa njia ya video. 
 
Katika ukurasa huu, Habari za UN itakupatia kiti cha mbele kabisa kutoka kwenye kumbi zote. Kupitia simu yako ya kiganjani au rununu bila kusahau kompyuta yako au kishkwambi, utafuatilia hotuba za wakuu wa nchi na serikali wakati wakitoa ainisho au majawabu ya changamoto zinazokabili Dunia hivi sasa, sambamba na wanavyoshiriki katika mkutano wa ngazi ya juu wa Marekebisho ya Mfumo wa Elimu, kushughulikia janga la chakula duniani, maadhimisho ya miaka 30 ya Azimio la UN kuhusu haki za watu wa makabila madogo halikadhalika mzozo wa Ukraine.

Rambaza kwenye majukwaa yetu ya mitando ya kijamii

Twitter: Habari za UN
Youtube: Habari za UN

Taswira ya ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
UN Photo/Manuel Elías

UNGA77 yafunga pazia, Afrika yasema sasa ni wakati wa kuwa na ujumbe wa kudumu

Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA77 umekunja jamvi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ukiwa na maudhui: Wakati muhimu: Majawabu ya kuleta marekebisho kwa changamoto zinazofungamana. Katika siku 6 za mjadala huo nchi za Afrika zilitumia fursa kuhoji marekebisho gani yanawezekana bila kurekebisha chombo hicho ambacho kura  yenye maamuzi ya msingi inamilikiwa na wanachama 5 kati ya 193, ikiwa ni miaka 77 tangu kuudwa kwake.

27 Septemba 2022

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa kina na Mashinani.

Katika Habari kwa ufupi: Kurejea nyumbani kwa hiyari kwa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutoka nchini Zambia. Pili kutangazwa kutokomezwa kwa EBola nchini DRC na Habari ya Tatu ni kuhusu siku ya utalii duniani na wito kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka utalii wa aina mpya usioaharibu mazingira na wenye mnepo kwa kila mkazi wa dunia.

Sauti
13'48"