Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumeazimia kumaliza mzozo nchini mwetu na kutumia rasilimali kujikwamua- Rais Tshisekedi

Rais Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo  wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la UN
UN /Cia Pak
Rais Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la UN

Tumeazimia kumaliza mzozo nchini mwetu na kutumia rasilimali kujikwamua- Rais Tshisekedi

Amani na Usalama

Rais Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikigusia mambo kadhaa ikiwemo amani na usalama mashariki mwa taifa lake pamoja harakati za kuinua uchumi wa nchi kupitia rasilimali lukuki nchini humo.

Rais Tshisekedi amesema Umoja wa Mataifa unafahmamu kuwa DRC ni muathirika wa janga kubwa la usalama lililodumu Mashariki mwa nchi kwa zaidi ya miaka 20.

Sio siri rasilimali tulizo nazo ndio chanzo cha mzozo

“Amesema mfuatiliaji yeyote wa dhati akizungumza kwa nia njema atakubali kuwa sababu sio ya mzozo Mashariki mwa DRC unachochewa na rasilimali zilizomo ndani ya taifa hilo,” amesema Rais Tshisekedi.

Amesema wananchi wa DRC wanatambua mchango wa Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, Jumuiya za kikanda za Afrika, Muungano wa Ulaya na wadau wengine katika kukabili janga hilo lilalojirudia mara kwa mara.

Zaidi ya yote amesema “tunatambua kujitoa kwa walinda amani jasiri wa Umoja wa Mataifa ambao wamepoteza maisha yao wakitetea maadili ya amani na haki.”

Hata hivyo amesema, licha ya juhudi za ndani, uwepo wa walinda amani wa UN wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja huo, MONUSCO pamoja na msaada wa kidiplomasia kwa miaka 23, ukosefu wa usalama unazidi kutishia taifa lake.

Mambo matano ya kusaidia kujenga amani ya kudumu DRC

Rais Tshisekedi ameomba Umoja wa Mataifa, Muungano wa AFrika, Jumuiya za kikanda ya Afrika na wadau wa DRC kusaidia kujenga upya usalama, amani ya kudumu na kuweka mazingira bora ya kuweka ushirikiano wenye matunda kwa maslahi ya wakazi wote wa ukanda wa Maziwa Makuu.

Ili kufanikisha hilo amesema ni kutekeza mambo matano ikiwemo: mosi kuondoka kwa kikundi cha waasi cha M23 kwenye maeneo waliyoko na wakimbizi wa ndani kurejea kwenye makazi yao. Pili kusaidia kutekeleza kwa makubaliano ya Nairobi na kupeleka kwa walinda amani kutoka Afrika Mashariki.

Ondoeni vikwazo dhidi ya jeshi la DRC ili lifanye kazi yake

Suala lingine ni "ondoeni vikwazo vyote vya kuwezesha serikali ya DRC kurekebisha jeshi lake la ulinzi,  kuongeza mamlaka yake ili liweze kufanya kazi yake vizuri, ikiwemo kuondoka hatua zote zinazokwamisha kupata vifaa vya kijeshi bila kujali mifumo iliyowekwa na Baraza la Usalama."

Rais Tshisekedi amesema wanataka utulivu wa kudumu ili kuweza kutumia rasilimali zilizoko kwa maslahi ya wananchi na ukanda mzima wa Maziwa Makuu.

Mkataba wa DRC na Zambia kuchakata madini bila uchafuzi

Amesema DRC ni miongoni mwa wazalishaji wakuu wa madini muhimu kwenye kipindi cha mpito cha kuondokana na nishati kisukuku. Madini kama vile Lithium, Kobalti, Nickel, Manganese, na wameamua kuchakata madini hayo bila kuharibu mazingira, na hvyo mwezi Aprili mwaka huu, DRC na Zambia walitia saini mkataba wa kuanzisha mnyororo wa thamani kwenye sekta ya betri za umeme na sekta ya nishati salama.

Amesema kwa kuzingatia ukubwa wa mradi, ushiriki wa wabia hususan kwenye mtaji na teknolojia itakuwa ni muhimu.