Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA77

MKUTANO WA 77 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Pata habari kutoka UNGA77

Mambo sasa yameiva kwa ajili ya Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wakati dunia inaanza taratibu kujikwamua kutoka katika janga baya kabisa la coronavirus">COVID-19, mjadala wa ngazi ya juu wa mkutano wa 77 kwa kiasi kikubwa utafanyika kwa viongozi kuweko kwenye ukumbi mashuhuri wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, tofauti ya miaka miwili iliyopita ambapo viongozi wengine walikuweko ukumbini na wengine walitoa hotuba zao kwa njia ya video. 
 
Katika ukurasa huu, Habari za UN itakupatia kiti cha mbele kabisa kutoka kwenye kumbi zote. Kupitia simu yako ya kiganjani au rununu bila kusahau kompyuta yako au kishkwambi, utafuatilia hotuba za wakuu wa nchi na serikali wakati wakitoa ainisho au majawabu ya changamoto zinazokabili Dunia hivi sasa, sambamba na wanavyoshiriki katika mkutano wa ngazi ya juu wa Marekebisho ya Mfumo wa Elimu, kushughulikia janga la chakula duniani, maadhimisho ya miaka 30 ya Azimio la UN kuhusu haki za watu wa makabila madogo halikadhalika mzozo wa Ukraine.

Rambaza kwenye majukwaa yetu ya mitando ya kijamii

Twitter: Habari za UN
Youtube: Habari za UN

20 SEPTEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anakuletea jarida likianza na Habari kwa Ufupi ikianza na ufunguzi wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu Antonio Guterres akitaka ubia wa kimataifa kukabili mgawanyiko unaozidi kushamiri kila uchao. Kisha Rais wa Brazil  na kwingineko kutangazwa kwa mlipuko wa Ebola aina ya Sudan nchini Uganda.

Mada kwa kina ni kuhusu kijana mkimbizi anayesoma Canada ambaye amenuia kuwasaidia wenzake aliowaacha katika kambi za Kakuma na Dadaab nchini Kenya.

Sauti
12'23"
Katibu Mkuu wa UN António Guterres akihutubia ufunguzi wa mjadala mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la UN
UN /Cia Pak

Tunahitaji ubia wa dunia wakati huu ambao mgawanyiko unazidi- Guterres

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu Antonio Guterres amezungumza wakati wa ufunguzi akigusia masuala lukiki ikiwemo mgawanyiko wa kisiasa na kijiografia duniani, mizozo, uhaba wa chakula, ongezeko la gharama ya maisha, mabadiliko ya tabianchi na teknolojia akisema maendeleo yaliyofikiwa katika Nyanja mbali mbali yanakwamishwa na mgawanyiko wa kisiasa na kijiografia.

Watoto wakiwa wameketi kimduara na mwalimu wao katika kituo cha awali cha maendeleo ya mtoto kwenye kijiiji cha Garin Badjini, kusini-mashariki mwa Nigeria
© UNICEF/Giacomo Pirozzi

Jiulize bila elimu ungalikuwa wapi? Lakini kwa watoto maskini bado elimu ni ndoto- Guterres

Bila elimu ningalikuwa wapi? Tungalikuwa wapi wengi wetu humu ndani?  Ndivyo alivyoanza hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati akihutubia viongozi walioshiriki kikao cha ngazi ya juu cha mkutano wa marekebisho ya mfumo wa elimu duniani, kikao kilichofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

UN/Anold Kayanda

Sasa ni wakati wa kutekeleza maneno yetu kwa vitendo, asema Emmanuel Msoka akiwa UNGA77

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu leo unakunja jamvi kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani. Mkutano huo wa siku tatu umeitishwa ili kukabiliana na changamoto ya kimataifa ya elimu hasa kwa kuzingatia suala la usawa na ujumuishwaji, ubora wa elimu na umuhimu.  

Wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa nchi na serikali, mashirika ya kimataifa na makundi mbalimbali katika jamii wamepata fursa ya kupaza sauti zao, miongoni mwao ni vijana walioshiriki kuwawakilisha mamilioni ya wanafunzi kote duniani.  

Sauti
2'23"

19 SEPTEMBA 2022

Hii leo kwenye Habari za UN, Flora Nducha anaanza na Kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, akisema elimu ndio kitu ambacho kinaweza kuleta amani na maendeleo ya kudumu duniani. Kisha ni taarifa ya mahojiano na mchechemu wa vijana wa UNICEF nchini Tanzania, Emmanuel Msoka akisema “maneno ni rahisi lakini vitendo ni aghali,” hivyo vitendo vyahitajika ili kusongesha maendeleo ya kweli. Anapendekeza kurejeshwa kwa Baraza la Vijana nchini Tanzania.

Sauti
12'4"