Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna taifa lililo bora kuliko lingine, mshikamano wa kimataifa ni muhimu:China

Waziri wa mambo ya nje wa jamhuri ya China Wang Yi akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu UNGA77
UN Photo/Laura Jarriel
Waziri wa mambo ya nje wa jamhuri ya China Wang Yi akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu UNGA77

Hakuna taifa lililo bora kuliko lingine, mshikamano wa kimataifa ni muhimu:China

Masuala ya UM

Kila mtu katika hii dunia anategemea amani ili kuweza kuishi, kuwa huru, kuwa na maendeleo na kufurahia maendeleo hivyo ni jukumu la kila mtu na kila nchi kuidumisha amesema Wang Yi Waziri wa mambo ya nje wa China akiwasilisha hotuba yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza Kuu hii leo mjini New York Marekani.

Katika hotuba yake Bwana Yi amesisitiza mambo sita muhimu akisema endapo tayazingatiwa basi dunia itakuwa mahala bora zaidi pa kuishi kwa kila mtu, kila nchini duniani kote.

Mosi:amesema “Ni lazima tudumishe amani na usalama kwani wote tunaitegemea ili kufanikisha malenmgo yetu ya kitaifa na kimataifa.”

Amesisitiza kuwa maendeleo na fanikio hayawezi kupatikana andapo kuna vita, mivutano na migogoro ambayo inawalimisha amamilioni ya watu kufungasha virago na kukimbia makazi yao, kwani hawawezi kuchangia chochote katika maisha yao nan chi zao.

Pili:Amesema “Ni lazima tuhakikishe kuna maendeleo na tukomeshe umasikini.” Amesema China ikiwa ni moja ya mataifa yanayoendelea inaamini kwamba hakuna maendeleo ya kweli duniani iwapo asilimia kubwa ya watu bado wanaishi katika umasikini mkubwa. 

Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kwamba maendeleo ya dunia yanakuwa yenye usawa na jumuishi ili kuhakikisha ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s haimuachi yeyote nyuma.

Tatu: Bwana Yi amesema “Ni lazima tuwe wazi , kuhakikisha ujumuishwaji na kuzingatia sheria za biashara za kimataifa zilizowekwa na shirika la biashara la kimataifa WTO.”

Ameendelea kusema kwamba ubinafsi na mivutano ya kibiashara haimnufaishi yeyote bali inaongeza shinikizo kwa watu, nchi na jumuiya ya kimataifa.

 Nne: Amesema “Lazima tukumbatie ushirikiano na kuepuka mivutano na ushirikiano uwe wa kufaidisha pande zote”

Katika hilo Bwana Yi amesema ushirikiano uwe katika ngazi ya nchi nan chi , nchi na mashirika au ushirikiano wa kimataifa unapaswa kuheshimu pande zote na kuleta tija kwa pande zote, hakuna anayestahili kufaidika zaidi ya mwingine katika ushirikiano wowote akitolewa mfano wa ushirikiano mzuri uliopo baina ya China mataifa mengi ya nchi zinazoendelea.

Tano: Amesema ni “Lazima tudumishe mshikamano na kuepuka mivutano , ubaguzi na migawanyiko na kushirikiana kuchagiza maendeleo kwa wote.”

Na sita: waziri huyo wa mambo ya nje amesema “Tuheshimu usawa na kuepuka uonevu, hakuna nchi iliyo juu ya nyingine na inayostahili kuonea nyingine. Tujenge msimamo wa pamoja na kunyoosha mkono kuwasaidia wasiojiweza.”

Amesema China imejitajhidi kufuta na kupunguza madeni hasa ya nchi zinazoendelea ili kuzisaidia kusonga mbele katika SDG’s.

Na katika kudumisha amani na kuheshimu miakataba ya kimataifa amesema “China ni nchi pekee miongoni mwa wanachama watato wa kudumu ambayo inamiliki nyuklia iliyoahidi kutotumia silaha hizo”

Maendeleo na misaada

Waziri huyo wa mambo ya nje amesema China imekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo na ni mshirika wa maendeleo katika nchi takribani 130 kote duniani.

Amesema pia China imekuwa mbele kwa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ambapo imepiga hatua miaka 10 zaidi ya wengine.

Mbali ya hayo amesema China imekuwa mdau mkubwa wa ushirikiano wa kimataifa kwa kutekeleza karibu mikataba yote iliyowekwa na chi wanachama wa Umoja wa Mataifa .

Na kwa kushirikiana na nchi zingine zinazoendelea China imekuwa sauti ya wasio na sauti.

Mambo mengine aliyogusia ni pamoja na hali ya Afghanistan ambayo amesisitiza suluhu ni kuweka mkakati Madhubuti wa kuhakikisha amani ya kudumu.

Katika suala la uhakika wa chakula amesema ni tioshio kote duniani na ndio maana China imeweka m ikakati Madhubuti ya kulinda watu wake dhidi ya zahma hiyo huku ikinyoosha mkono kuwasaidia ambao tayari wamesathirika.

Amesema mwaka huu pekee imetoa tani 1500 za msaada wa chakula kwa ajili ya nchi zinazoendelea zilizpoathirika na kutokuwa na uhakika wa chakula.

Kuhusu mzozo wa Ukaraine amesema "China inaunga mkono juhudi za mazingira ya amani ya utatuzi wa mgogoro wa Ukraine. kipaumbele kikubwa ni kuwezesha mazungumzo ya amani. Suluhisho la msingi ni kushughulikia hofu za maswala halali ya usalama ya pande zote na kujenga mfumo wenye uwiano, ufanisi na endelevu.

Janga la COVID-19

Kuhusu COVID-19 Waziri Yi amesema China ambayo bado inakabiliana na janga la COVID-19 inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha inalinda watu wake na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.

China imekuwa miongoni mwa nchi za kwanza na hasa katika nchi zinazoendelea kuzalisha chanjo ya COVID-19 sio tu kwa watu wa China lakini pia kwa manufaa ya dunia na hasa nchi zinazoendelea kwani chanjo yake ni ya gharama nafuu sababu inaamini kwamba kila mtu katika kila nchi anastahili kufikiwa na chanjo.

Suala la Palestina

Kuhusu suala la Palestina China imesema inaamini suluhu pekee ni kuwa na mataifa mawili yanayoishi kwa amani na usalama na itaendelea kuchagiza Umoja wa Mataifa na wanachama wengine kuhakikisha suluhu ya mateso ya Wapalestina yanamalizwa.

Ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuwasaidia mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina China itaendelea kusaidia mashirika ya kibinadamu yanayofanyakazi bila kuchoka kutoa msaada wa kuokoa maisha ya wapalestina.

Waziri huyo pia amezungumzia suala la Kisiwa cha Taiwani akisistiza kuwa bado taifa hilo linapigania kukijumuisha tena katika taifa la China kwani inaamini ni sehemu yake. 

Ameongeza kuwa China itaendelea kutumia njia za amani kuhakikisha azma hiyo inatimia kwani inaamini watu wa Taiwani na China ni wamoja na wanastahili kuwa taifa moja.

Pia amesema ushirikiano wa Kusini-Kusini ni muhimu sana kwa China na mataifa mengine yanayoendelea hivyo ni vyema ukaendelea kudumishwa.