Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fursa iko hapa na sasa tuchukue hatua: Asema Kőrösi' akihutubia UNGA77

Rais wa Baraza Kuu la UN Csaba Kőrösi' akihutubia ufunguzi wa Mjadala Mkuu wa UNGA77
UN /Cia Pak
Rais wa Baraza Kuu la UN Csaba Kőrösi' akihutubia ufunguzi wa Mjadala Mkuu wa UNGA77

Fursa iko hapa na sasa tuchukue hatua: Asema Kőrösi' akihutubia UNGA77

Masuala ya UM

Mambo yanakuwa mazuri  pale tunapoyaboresha, na mambo yanaenda mrama pale tunaposhindwa kutumia fursa iliyo mbele yetu, ndivyo alivyotamatisha hotuba yake hii leo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi' wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mjadala mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Bwana Kőrösi' amesema ametumia msemo huo kwa kutambua kuwa changamoto zinazokabili dunia hivi sasa zimesababisha hali kuwa ngumu, lakini dunia itakuwa bora iwapo hatua zikichukuliwa na itaenda mrama kama hatua zitapuuzwa.

Amesema “fursa iko hapa na sasa. Hebu tuchukue hatua.”

Svitlana kutoka eneo lililoathiriwa na migogoro mashariki mwa Ukraine alipokea kuku wa siku 30 kwa ajili ya ufugaji wa aina mbili.
© FAO/Viktoriia Mykhalchuk
Svitlana kutoka eneo lililoathiriwa na migogoro mashariki mwa Ukraine alipokea kuku wa siku 30 kwa ajili ya ufugaji wa aina mbili.

Mshikamano, Uendelevu, Sayansi

Rais huyo ametaja fursa hizo kuwa ni pamoja na nyaraka na mikataba mbalimbali ya kimataifa iliyopitishwa kuleta majawabu, akisema, ndio maana dunia inahitaji majawabu kupitia mshikamano, uendelevu na sayansi.

Majawabu kwa sababu tayari tumeandika mikataba mingi, tumeweka malengo mengi lakini hatua tunazochukua ni kidogo. Mshikamano kwa sababu kiwango cha ukosefu usawa kimevunja rekodi. Uendelevu kwa sababu tunataka kuacha dunia bora kwa vizazi vijavyo, na sayansi kwa kuwa inatoa Ushahidi usioegemea upande wowote kwa vitendo vyetu.

Vitendo kama vile vinavyozidi kuchangia kwenye mabadiliko ya tabianchi, vita, mizozo, magonjwa na vita.

Mchoro kwenye moja ya kuta nchini Colombia ukiwa na maneno "maridhiano na manusura" ukionesha maendeleo ya kitamaduni katika kujumuisha wapiganaji wa zamani wa kikundi cha FARC nchini Colombia
UN Mission in Colombia/Bibiana Moreno
Mchoro kwenye moja ya kuta nchini Colombia ukiwa na maneno "maridhiano na manusura" ukionesha maendeleo ya kitamaduni katika kujumuisha wapiganaji wa zamani wa kikundi cha FARC nchini Colombia

“Nani alitarajia kuwa vita ingalirejea tena Ulaya?” amehoji Bwana Kőrösi' na kwamba tishio la nyuklia lingarejea kwenye mijadala ya kisiasa kusaka suluhu ya mgogoro na jirani.

Amesema maudhui ya mkutano wa UNGA77; Wakati muhimu: Majawabu ya kuleta mabadiliko katika changamoto zinazoingilia yanalenga kuleta ahueni kwa wakazi wa dunia kuanzia walioathiriwa na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi kama vile mafuriko Pakistani.

Majawabu kutoka kwenye hadubini kwenda kwenye vipazasauti

Amesema majawabu ya kisayansi yalitolewa na Jopo la Kimataifa kwa mabadiliko ya tabianchi, akisema chombo hicho kimedhihirisha kuwa mbinu bora ya kusaidia kutekeleza maamuzi ya kisiasa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuhimili madhara yake.

“Tunapaswa kusambaza mafanikio yake kwenye maeneno ya maji, nishati, chakula na bayonuai,” amesema Kőrösi'akiongeza kuwa baada ya wiki ya mjadala mkuu ataanzisha msururu wa mashauriano na jamii ya wanasayansi “nikiwaomba watusaidie.”

Amesema mashauriano hayo yatasaidia “kutoa majawabu kwenye hadubini na kuyapeleka kwenye vipaza sauti.”

Mtoto akichota maji kwenye chanzo ambacho kinamaji kidogo kutokana na ukame uliokausha maziwa huko Dollow Somalia
© UNICEF/Sebastian Rich
Mtoto akichota maji kwenye chanzo ambacho kinamaji kidogo kutokana na ukame uliokausha maziwa huko Dollow Somalia

Pande tatu za matatizo kuhusu maji: Mengi, hayatoshi, si salama

Amezungumzia pia mkutano wa mwaka ujao kuhusu Maji, wa kwanza tangu mwaka 1977 akisema “maji yanatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha mzozo duniani kote.”

Matatizo ya maji ni pande tatu: Mengi, hayatoshi, si salama.

Bwana Kőrösi' amesema kupitia mkutano huo wana fursa ya kuleta mabadiliko chanya kwa maisha ya watu zaidi ya bilioni 2.1 ambao hawana fursa ya kupata maji safi na salama.

Amekumbusha kuwa zana za kuleta mabadiliko yenye marekebisho zipo: Ajenda 2030, Mkataba wa Parisi wa Mabadiliko ya Tabianchi, Mkataba wa Sendai, Programu ya utekelezaji ya Addis Ababa na Ajenda yetu ya Pamoja.