Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biden amelaani ukiukaji wa Urusi usio na aibu wa Mkataba wa UN, na kuutaka ulimwengu kusimama na Ukraine

Rais  Joseph R. Biden wa Marekani akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 77
UN Photo/Cia Pak
Rais Joseph R. Biden wa Marekani akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 77

Biden amelaani ukiukaji wa Urusi usio na aibu wa Mkataba wa UN, na kuutaka ulimwengu kusimama na Ukraine

Amani na Usalama

Akilaani vikali uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, Rais wa Marekani Joe Biden ameonya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwamba "ikiwa taifa linaweza kufuata matamanio yake bila bila kuwajibishwa, basi tunaweka hatarini kila kitu ambacho taasisi hii kubwa inasimamia."

Katika ufunguzi wa hotuba yake iliyosheheni hii leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Biden amesema kuwa katikati ya misukosuko mingi ambayo ulimwengu umeshuhudia katika mwaka uliopita kuanzia mabadiliko mabaya ya tabianchi hadi janga linaloendelea la COVID-19 na kuongezeka kwa uhaba wa chakula na mafuta " mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alimvamia jirani yake, alijaribu kufuta taifa huru kutoka kwenye ramani."

Ameendelea kusema kwamba "Urusi imekiuka bila aibu kanuni za msingi za mkataba wa Umoja wa Mataifa na leo tu Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa vitisho vya wazi vya nyuklia dhidi ya Ulaya akipuuza na kutojali msimamo wa kimataifa wa kutoeneza silaha za nyuklia.” 

Bwana. Biden pia amesema Urusi "hivi sasa inaita wanajeshi zaidi na kuandaa kura ya maoni ya isiyo na maana juu ya unyakuzi wa ardhi ambayo tayari inamiliki mashariki mwa Ukraine.”

Vita vya kikatili na visivyo na maana

Rais huyo wa Marekani ameendelea kusema kwamba "Ulimwengu unapaswa kuona vitendo hivi jinsi vilivyo, hakuna mtu ambaye ametishia Urusi. Urusi ilitafuta mzozo huu. Mtu mmoja alitafuta vita hivi vya kikatili, visivyo na maana. Vita hivi ni vya kuzima haki ya taifa la Ukraine kuwa nchi, ni bayana na rahisi, na haki ya Waukraine kuishi kama watu.”

Ameongeza kuwa "Popote ulipo, popote unapoishi, chochote unachoamini . Hilo linapaswa kufanya damu yako iwe baridi," ameendelea, akiongeza kwamba Baraza Kuu lilishutumu uchokozi wa Urusi na zaidi ya nchi 140 katika chumba hiki leo ziliunga mkono mkutano mkuu unaolaani Urus, uchokozi wake dhidi ya Ukraine, wakati Marekani ilikuwa imeongeza kiwango kikubwa cha uungaji mkono kwa nchi hiyo, na imetoa zaidi ya dola milioni 25 hadi sasa. 

Bwana Biden amesema kuwa nchi yake imeonya kuhusu uvamizi huo na ilijitahidi  kwa bidii kuepusha vita.

"Kama mlivyo wengi wenu, Marekani inataka vita hivi viishe na kumalizika kwa masharti ya haki, na kuzitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuwa wazi na bila kuyumbayumba katika azimio lenu la kushikilia kanuni za mkataba wa Umoja wa Mataifa kwamba Ukraine ina haki sawa na nchi yoyote au taifa jingine huru. Tunasimama kwa mshikamano dhidi ya uchokozi wa Urusi, huwezi kukamata eneo la nchi nyingine kwa nguvu. Nchi pekee inayofanya hivyo ni Urusi.”

Panuawigo wa demokrasia na haki za binadamu kwa mustakbali bora

Rais Biden ameendelea kusema kwamba Marekani itaendelea kutetea na kutetea demokrasia duniani kote kwa sababu inaamini demokrasia kuwa ni chombo kikubwa zaidi cha kutatua changamoto za wakati wetu na itafanya kazi ndani ya G7 na nchi nyingine zinazofanana ili kuthibitisha kwamba demokrasia inaweza kukidhi mahitaji kwa ajili ya raia wake na kutimiza kwa ajili ya dunia nzima.

"Taasisi hii, inaongozwa na mkataba wa Umoja wa Mataifa na azimio la kimataifa la Haki za Kibinadamu, kama kitovu chake na kuwa ni kitendo cha matumaini yasiyotisha, na Marekani daima itatetea haki za binadamu, kwani ni msingi wa yote tunayotaka kufikia." 

Mustakbali bora utafikiwa nan chi ambazo zinatoa fursa kwa watu wake kufikia uwezo wao wa mafanikio.

Lakini akaonya kwamba hata Baraza kuu lilipokuwa likikutana "Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambao ni msingi wa utulivu wa kimataifa, unashambuliwa na wale wanaotaka kuuvunja au kuupotosha kwa manufaa yao wenyewe." Kwa hivyo, Marekani itaendelea kusimama na kanuni za Umoja wa Mataifa. "Hili ni jukumu la kila nchi mwanachama."

Wakati huo huo, amesema “Marekani inaamini kwamba Umoja wa Mataifa unapaswa kuchukua hatua zaidi za kurekebisha michakato na mbinu zake za kufanya kazi na hasa ili iwe jumuishi zaidi ili iweze kuwa mwakilishi zaidi wa ulimwengu tunamoishi."

Ameongeza kuwa Baraza la Usalama lazima vile vile lifanyiwe mageuzi ili kujumuisha wanachama zaidi wa kudumu na wasio wa kudumu. 

Wanachama wa Baraza la Usalama pia wanapaswa "kutetea mkataba wa Umoja wa Mataifa mara kwa mara na kujiepusha na matumizi ya kura ya turufu isipokuwa katika hali ya nadra, isiyo ya kawaida."

Kuhusu China

Rais Biden amesema "Wacha niseme kinagaubaga kuhusu ushindani kati ya Marekani na Uchina. Tunapodhibiti mabadiliko ya mwelekeo wa kisiasa wa kijiografia, Marekani itajiendesha kama kiongozi anayefaa. Hatutafuti migogoro, hatutafuti vita baridi. Hatuulizi taifa lolote kuchagua kati ya Marekani au mshirika mwingine yeyote. Lakini Marekani haitaaibishwa kwa kukuza maono yetu ya ulimwengu huru, wazi, salama na ustawi na kile tunachoweza kutoa  kwa jumuiya za mataifa.”

Na juu ya Taiwan, amesema kuwa Marekani inataka kudumisha utulivu na amani katika eneo hilo na kuongeza kuwa "tunaendelea kupinga mabadiliko yanayoegemea upande mmoja katika hali ilivyo kwa kila upande."