Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 SEPTEMBA 2022

22 SEPTEMBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anakuletea mada kwa kina, Habari kwa Ufupi na Neno la Wiki.

Habari kwa Ufupi zinamulika harakati za kutumia chanjo inayoweza kukabili virusi aina ya #EbolaSudan nchini Uganda kwa kuwa chanjo ya sasa haina uwezo huo. Pia nafasi ya nishati jadidifu katika kuongeza ajira duniani, ripoti mpya imethibitisha hilo! Kisha wito wa Rais wa Botswana kwenye mjadala mkuu wa UNGA77 wa kutaka wananchi wake nao waajiriwe Umoja wa Mataifa.

Mada kwa kina ni kauli ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki kuhusu ombi la Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix-Antoine Tshisekedi ya kupelekwa jeshi la kanda ya Afrika Mashariki nchini mwake ili kulinda amani.

Neno la wiki leo kutoka BAKITA, Mhariri Mwandamizi Onni Sigalla anafafanua maana ya neno Mzishi.

Karibu!

Audio Credit
FLORA NDUCHA
Audio Duration
12'36"