WHO imetaka serikali duniani ziokoe maisha ya watu milioni 50 wanaougua magonjwa yasiyoambukiza, NCDs

WHO imetaka serikali duniani ziokoe maisha ya watu milioni 50 wanaougua magonjwa yasiyoambukiza, NCDs
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa ulimwengiuni WHO leo kandoni mwa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York Marekani limezindua ripoti mpya inayowataka viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs ambayo hukatili Maisha ya watu milioni 17 kila mwaka.
Akizundua ripiti hiyo mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “Ripoti hii ni kumbusho la tishio kubwa linaloletwa na NDCs na hatari zake. Kuna hatua ambazo ni za gharama nafuu ambazo kila nchi bila kujali kiwango chake cha kipato kote duniani zinaweza na zinapaswa kuzichukua na kufaidika nazo kuanzia kuokoa maisha ya wat una kuokoa gharama. Namshukuru Rais Afuko-Addo , Waziri mkuu Store na Michael Bloomberg kwa uongozi wao na maono yao katika kushughulikia changamoto za kimataifa za afya.”
Ili kusongesha mchato huo wa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo, Kkisukari, saratani, magonjwa ya mfumo wa hew ana mengineyo, WHO imemteua tena kwa mud awa miaka mingine miwili Michael Bloomberg kama balozi wa kimataifa wa WHO kwa ajili ya NDCs, ukiwa ni muhula wake wa tatu.

Akikubali jukumu hilo kwa muhula mwingine Bwana Bloomberg amesema” Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama magonjwa ya moyo, kisukari, matatizo ya mapafu na saratani ni wauaji wakubwa wa kimyakimya lakini mara nyingi yanaweza kuzuilika kwa ufadhili unaostahili na hatua zingine ambazo si za gharama kubwa. Niko tayari kuendelea kuchagiza uwekezaji wa kuokoa Maisha kwa NCDs na kufanyakazi bega kwa bega na Dkt. Tedros.”
WHO imesisitiza kuwa bado uelewa wa umma kuhusu uhusiano uliopo baina ya NCDs na hatari ya vichocheo vyake kama matumizi ya tumbaku na pombe , lishe duni na kutofanya mazoezi ni mdogo sana. Hivyo limezitaka nchi kuongeza juhudi katika upande huo pia.
Shirika hilo la afya linasema lengo kubwa ya ripoti ya sasa na wito wake ni kuhakikisha hatua zitakazochukuliwa zinaokoa Maisha ya watu milioni 50 ifikapo mwaka 2030 kote duniani .